NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.


Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddy Hassan Kimanta  amelaani kitendo kiovu cha udanganyifu uliofanywa na shule tatu  binafsi za msingi mkoani humu katika mtihani wa darasa la saba na kupelekea matokeo ya wanafunzi kufutwa.


Kimanta alilaani kitendo hicho wakati akifungua kikao cha uchaguzi wa wanafunzi waliofaulu mtihani wa kumaliza elimu ya nsingi na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2021.Kimanta alisema kuwa  kitendo hicho kimeharibu sifa ya Arusha na kufanya miaka saba ya watoto ambao matokeo yao yamefutwa kuwa bure  jambo ambalo halikubaliki ambapo shule hizo ni shule za mchepuo wa kingereza ya Precious ya halmashauri ya Meru, Eunoto ya wilaya ya Monduli pamoja na Dominion ya Arusha Jiji.


“Jambo hilo halikubaliki limepelekea watoto kupata adhabu ya kufutiwa matokeo kwa kuponzwa na watu wazima wanahitaji sifa wasizostahili,”Alisema Kimanta.


Alieleza kuwa ili wapate sifa wafundishe wafundishe kama ambavyo taratibu na kanuni zinavyoelekeza na sio kufanya vitendo viovu vinavyoleta aibu na kuharibu sifa ya mkoa.


Alifafanua kuwa mkoa wa Arusha una mikakati mizuri ya kuhakikisha kiwango cha elimu kinapanda hivyo anatoa rai kwa shule binafsi kuhakikisha wanafuata taratibu na sheria na kutafakari wanatakiwa kufanya nini kwa maslahi ya taifa.


Kwa upande wake kaimu Afisa elimu mkoa wa Arusha Emmanuel Maundo mwaka 2014 jumla wanafunzi elfu 44,754 wavulana wakiwa elfu 22, 357 na wasichana elfu 22,447 walianza darasa la kwanza na waliosajiliwa kufanya mtihani wa darasa la saba walikuwa elfu 40,729 wavulana wakiwa ni elfu 20,059 na wasichana elfu 20,670.


Alieleza kuwa waliofanya mtihani ni wanafunzi elfu 40,192 wavulana wakiwa ni elfu 19,730 na wasichana 20,462 ambapo waliofaulu ni wanafunzi elfu 37,057 wavulana wakiwa ni elfu 17,864 na wasichana elfu 19,193 sasa na asilimia 92.42.“ufaulu umeongezeka kwa asilimia 0.75 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka 2019 ambao ulikuwa ni asilimia 91.67 ambapo kwa sasa ongezeko la wanafunzi waliofaulu ni elfu 2,548 na kupelekea ARUSHA kushika nafasi ya pili kitaifa,” Alisema.


Naye katibu tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega alisema kuwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa awamu ya kwanza ni wanafunzi elfu 34,263 wasichana wakiwa ni elfu 17,762 na wavulana wakiwa ni elfu 16,501 sawa na asilimia 94.4 ambapo alama za ufaulu zilizochukuliwa ni 245 hadi 100.


Amefafanua kuwa waliobaki jumla ni elfu 2768 sawa na asilimia 5.6 ambao wataingia kwenye chaguo la pili baada ya kukamilika kwa miundo mbinu ya madarasa  February 28.


Hata hivyo kwa shule zilizofutiwa matokeo  shule ya Precious ni wanafunzi 23 wavulana wakiwa ni 12 na na wasichana 11, Dominion 52 wavulana wakiwa ni 21 na wasichana 30 na Eunoto  23 wavulana wakiwa ni 12 na wasichana 11.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: