Mkuu wa Mkoa  wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi,  akifunga mafunzo ya siku sita ya watu wenye kuishi na mambukizi ya vvu,yalioyo fanyika walayani Manyoni.
 Mkurugenzi wa Utafiti wa NACOPH,  Pantaleo Shoki akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Watu wanaoishi na VVU wakisikiliza hutuba ya mkuu wa mkoa.
Na Ismaily Luhamb, Singida.

WATU waishio na Virusi vya Ukimwi (VVU) Mkoani Singida wametakiwa kuacha kutumia pombe.

WATU waishio na Virusi vya Ukimwi (VVU) Mkoani Singida wametakiwa kuacha pombe kwani pombe sio sehemu ya kupunguza mawazo na badala yake wafanye kazi kwa bidii  kujiongezea kipato wao na taifa kwa ujumla.

Akizungumza mbele ya mkuu wa mkoa wa Singida wakati wa kufunga mafunzo ya siku sita ya  TUYAJENGE , Mkurugenzi wa Utafiti wa NACOPH,  Pantaleo Shoki wanaoratibu mradi huo amemuhakikishia kuwa wataendelea kushirikiana serikali ili kuhakikisha kuwa Malengo ya Mradi huo yanatimia kama yalivyopangwa.

Shoki alisema mradi huo  unalenga kufikia mkakati wa Shirika la Umoja wa Kimataifa la Kupambana na Ukimwi (UNAIDSU ) wa 95-95-95 yaani asilimia 95 ya watu wote wanoishi na mambukizi ya VVU wewe wamepima na kugundua Afya zao,asilimia 95 ya watu waliopimwa na kukutwa na maambukizi wawe  wameanza tiba na asilimia 95 walio kwenye tiba wawe wamefubaza virusi hivyo ifikapo 2030.

Aidha Mkuu wa mkoa huo,  Dkt. Rehema Nchimbi aliwataka watu kuacha kudangayika na kushinda makanisani na kuacha kufanya kazi za kujiingizia kipato. 

"Ni kweli tutafute Mungu ila tuache unyanyapaa hauna faida yoyote kwetu sasa twende tukabadilike sasa na tufanye kazi ili tujiongezee kipato." alisema Dkt.Nchimbi na kuongeza.

"Natamani sana kama serikali ingetenga fungu kwa ajili ya watu wenye VVU kupatiwa mikopo kama watu wenye ulemavu na makundi mengine.hivyo nyinyi watu wa maendeleo ya jamii ishaurini serikali ili hawa watu waweze kupata mikopo kwa lengo la kujiongezea kipato."

Mpaka sasa hapa Tanzania kuna jumla ya mabaraza ya watu waishio na VVU 176, hivyo fikirini kuweza kuwapatia mikopo kupitia serekali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dkt.Nchimbi alisema takwimu zinaonyesha jumla ya watu laki sita na arobaini hapa nchini wanaoishi na Virusi vya Ukimwi wamejiunga na mabaraza ya konga, hivyo wakipatiwa mitaji tutaondakana na umaskini pamoja na  unyanyapaa.

Aliiagiza idara ya maendelo ya jamii Mkoani hapa kulipeleka hili kwa haraka kwa Mh.Rais ili aone namna ya kutusaidia kutupatia mikopo salama kwa watu hao.

Wakati hakitimisha hutuba yake Dkt. Nchimbi Amewatoa mashaka watu anoishi na VVU   kwa kuwataka wafanye kazi bila uoga, pia alitumia furusa hiyo kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa Tanzania kungia kwenye uchumi wa kati kabla ya mwaka 2025 na kusisitiza hana mpango wa kugombea ubunge kwani ameridhika na heshima aliyopewa na Rais ya nafasi aliyonayo ya ukuu wa mkoa.


Kaimu Mratibu wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Mkoa wa Singida, Jonathan Semiti alikiri kulipokea swala hilo ili kuona namna ya kuwapatia mitaji watu hao kwa kushirikiana na NACOPHA.

Akitoa salamu za mkoa Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Singida Dkt. Mohammed Mbalazi alisema kiwango cha mambukizi Mkoa wa Singida yameongezaka kutoka 3.3 hadi 3.6 sawa  na ongezeko la asilimia 0.3 na kuwa sababu kubwa ya ongezeko hilo ni  kuongezeka kwa miundombinu kama barabara na kuboreshwa.

Kwa upande wao washiriki wa semini hiyo wameishukuru Serikali ya Tanzania na watu wa Marekani kwa mradi huo wa kupunguza unyanyapaa hapa nchini.

"Tuna changamoto moja kubwa sisi watu tunaoishi na VVU,wengi wetu sio wa kweli hasa pale tunapo anza dawa wengi wetu hatuandiki majina ya kweli mwisho wa siku tunaipa tabu Serikali yetu kwa kututafuta ili tuende kuendelea kutumia dawa." alisema Salima Juma. 
Share To:

Post A Comment: