Muonekano wa jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo katika Wilaya ya Morogoro, ambalo linatarajiwa kuanza kutumika rasmi Aprili 15, mwaka huu.
Muonekano wa jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo katika Wilaya ya Morogoro (kulia) linalotarajiwa kuanza kutumika rasmi Aprili 15, mwaka huu na (kushoto) ni jengo linalotumika sasa na mahakama hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria wakitoka kukagua leo jengo la sasa la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo Wilaya ya Morogoro.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria wakiingia kukagua leo jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo Wilaya ya Morogoro. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria, Mhe. Emmanuel Mwakasala na (wa tatu kushoto) ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga, wa (kwanza kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Majengo ya Mahakama ya Tanzania, Mhandisi Khamadu Kitunzi.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Sifuni Mchome wakikagua leo jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo Wilaya ya Morogoro.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja leo na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria mara baada ya wajumbe hao kutembelea jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo Wilaya ya Morogoro. Wengine ni baadhi ya viongozi wa Mahakama ya Tanzania. (Picha na Magreth Kinabo – Mahakama)

Post A Comment: