Florah Mgonja Mratibu wa kazi za sanaa Kanda ya Kaskazini ,akiwa katika ofisi za Utamaduni Jijini Arusha
Na.Vero Ignatus,Arusha.
Mwisho
Na.Vero Ignatus,Arusha.
Baraza la
sanaa nchini lipo mkoani Arusha kwaajili ya kuratibu shughuli zote za sanaa
,kwa maana ya usajili na uratibu wa wadau kwa ujumla wakiwemo wamiliki wa
kumbi,bendi ,studio ,washehereshaji,DJ,waandaaji wa matamasha pamoja na matukio
mbalimbali ya sanaa kanda ya kaskazini.
Florah
Mgonja ni Mratibu wa kazi za sanaa Kanda ya Kaskazini amesema baraza hilo limeanzishwa kwa mujibu wa sheria
no 23 ya mwaka 1984 ,na kanuni zake za mwezi February 2018, zinawatambua
wasanii pamoja na kazi zao ,pia zinamtambua Afisa utamaduni kanuni ya mwaka
2018 kipengele cha 22,kinamtanbua Afisa huyo kuanzia ngazi ya wilaya hadi Taifa.
Amewataka
wasanii kwenda kujisajili ili waweze kuhudumiwa sambamba na kauli mbiu ya
Basata inavyosema kuwa sanaa ni kazi na kama zilivyo kazi nyingine hivyo ni vyema
wakajisajili ili watambulike .
Mgonja
amesema wasanii wengi wamekuwa wakilalamika kuwa wanasajiliwa na hawaoni
faida,watambue kuwa faida zipo nyingi kwani Basata lipo dawati ambalo msanii
hupewa fursa mbalimbali, na kazi zao namna zinaweza kulindwa kisheria.
“Vipo vinandaumiza vingi ambavyo
vinachukua kazi nyingi za wasanii,kama umesajiliwa serikali ipo kwaajili ya
kuangalia haki ya msingi ya msanii na tunaishughulikia kwa namna gani ili
msanii aweze kusonga mbele”alisema Flora.
Mratibu huyo
wa kazi za sanaa kanda ya kaskazini, amesema kuwa kwa sasa wapo wanatoa elimu
kwa wasanii na vikundi mbalimbali,ila wakati unakuja kwa wasanii ambao
hawatajisajili sheria itachukua mkondo wake .
Aidha
amesema Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kupitisha Sheria amabayo itawabana wasanii
ili kuwasaidia kiuchumi badala ile ya Mwanzo ya mwaka 1984 sheria No 23 kuwa na
mapungufu.
Florah
Mgonja ni Mratibu wa kazi za sanaa Kanda ya Kaskazini ,akisisitiza
jambo kwa waandishi wanhabari (hawapo pichani)katika ofisi Utamaduni Jijini Arusha.
Aidha amesema kulikuwa na malalamiko juu ya COSOTA,BODI YA FILAMU,BASATA kutokana na utendaji kazi wake kwani msanii alikuwa kote anatozwa kwa sasa serikali imaangalia namna gani hizi Taasisi tatu zinakuwa mamlaka ya usimamizi wa kazi za sanaa ambapo michakato tayari imeshaanza na inaratibiwa na TCRA.
Aidha amesema kulikuwa na malalamiko juu ya COSOTA,BODI YA FILAMU,BASATA kutokana na utendaji kazi wake kwani msanii alikuwa kote anatozwa kwa sasa serikali imaangalia namna gani hizi Taasisi tatu zinakuwa mamlaka ya usimamizi wa kazi za sanaa ambapo michakato tayari imeshaanza na inaratibiwa na TCRA.
Amesema kwa
wale wote a,mbao wanafanya kazi bila kusajiliwa sheria itafuata mkondo wake
kwasababu kwa sasa Basata ipo katika kuelimisha ,itafika mahali tukishaeka
mambo sawa ikiwemo sheria na hizi mamlaka kuwa pamoja ,tutahakikisha kuwa kila
anayejihusisha na shughuli za sanaa anasajiliwa.
Amesema zipo
faida nyingi za msanii kujisajili ikiwemo sheria,kazi zao kutunzwa kupata fursa
mbalimbali huku akiwataka wale ambao wameshajisajili kuhuhisha vibali vyao ,kwa
msanii binafsi ni shilingi 45,000 kwa vikundi 85,000 ikiwa imejumlishiwa na fomu.
Amebainisha
kuwa kwa sasa msanii hawezi kwenda nje ya kwa kupitia viwanja vya ndege nchi kama hajasajiliwa Basata,hivyo umuhimu
wa kujisajili ni mkubwa, kwani hata msanii akipata shida akiwa nje ya nchi ni
rahisi kusaidika kama amesajiliwa.
Amesema Basata
ipo kwaajili ya kushughulikia usajili kwa wasanii sambamba na ushauri wa namna
ambavyo wanavyoweza kuendesha shughuli zao za sanaa kwani fursa zipo nyingi
sana.
Aidha Basata
ilianza usajili kwa mwaka wa fedha 2018-2019 na usajili ulikuwa mzuri na wasanii
waliitikia kwa wingi,hivyo kwa mwaka huu wengi wanahuisha vibalivyao kwa wale
waliokwisha sajiliwa tayari ambapo wamekuwa mabalozi kwa wengine .
Ameeleza
kuwa kwasasa Basata imewarahisishia kazi wasanii,badala ya kwenda Jijini Dar es
salaam imewafuata hadi mkoa husika kwaajili ya kuwafanyia kushughulikia usajili
wao .
Hata hivyo
ameeleza kuwa msanii anapojisajili 25% ya makusanyo katika usajili huu unarudi
halmashauri kama sehemu ya uendelezaji wa shughuli za sanaa.
Mwisho
Post A Comment: