Kamati ya Siasa mkoa wa Arusha yaridhia utekelezaji wa miradi Wilayani Ngorongoro. Akizungumza baada ya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi  kwenye miradi ya maendeleo  ,Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Ndg.Lootha Sanare  ameipongeza Wilaya ya Ngorongoro kwa  kwa usimamizi mzuri wa utekelezaji  wa  miradi  katika sekta ya Afya,Maji na barabara ambayo  imekaguliwa na kamati hiyo ya CCM mkoa wa Arusha .       


Aidha Sanare amesema utekelezaji wa  Ilani ya chama cha mapinduzi unalenga kumpatia mwananchi huduma bora za afya,Maji ,Elimu na Mawasiliano,hivyo ameelekeza uongozi wa wilaya ya Ngorongoro kuhakikisha miradi  ambayo haijakamilika inakamilishwa mapema na wanachi kupata huduma.

Aidha Sanare ameutaka uongozi wa wilaya hiyo kutokusita kuwachukulia hatua watumishi watakaobainika kufanya ubadirifu wa fedha za miradi  sambamba kuwachukulia hatua za kisheria  wakandarisi wazembe wasiotekeleza matakwa ya mikataba yao kwa wakati.

Ziara hiyo ya Kamati ya Siasa mkoa wa Arusha imekamilika kwa kutembelea na kukagua miradi minne yenye thamani ya  shilingi zaidi  Bilioni 89 inayotekelezwa Wilaya ya Ngorongoro
Share To:

msumbanews

Post A Comment: