Mgombea wa ubunge kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM) John Daniel Pallangyo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa kuwa mbunge mteule wa Jimbo la Arumeru Mashariki.
Aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya chama cha Demokrasia Makini Simoni Paul Ngilisho akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushindwa kukidhi vigezo na sheria vya Tume ya Uchaguzi Taifa
Juma Mohameda alikuwa mgombea kwa tiketi ya chama cha ADATADEA akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya chama chake kushindwa kutimiza sheria na taratibu zinazohitajika kufuatwa.
Na. Vero Ignatus, Arumeru.
Aliyekuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM) John Daniel Palangyo amepita bila kupigwa katika uchaguzi mdogo wa jimbo la arumeru Mashariki.
Akimtangaza Mbunge huyo msimamizi wa Uchaguzi Emanuel Mkongo amesema kuwa hali hiyo inafuatia wagombea jumla ya wagombea 11 walichukuwa fomu ya kugombea ubunge wa jimbo hilo na wagombea Tisa wamerejesha fomu hizo huku wagombea watatu wakiwa hawajarejesha kabisa wengine kushindwa kujaza fpp} kwa usahihi hivyo kukosa vigezo.
Mkongo amesema Baadhi ya wagombea hao ambao wameshidwa kukidhi vigezo ni pamoja na wagombea watatu ambao hawakuteuliwa kwasababu hawajarudisha fomu ,huku wengine wakiwa saba wakiwa wamerejesha lakini hawakukidhi pamoja na kutolipa dhamana ya kugombea ubunge ambayo ni shilingi elfu 50 wadhamini pamoja na kuleta hati ya kula kiapo kutoka kwa mwanasheria na hakimu.
Msimamizi huyo wa uchaguzi amesema kuwa katika fomu hizo fomu moja tu ndio ambayo ilikuwa haina mapungufu ya kisheria hivyo alitumia nafasi hiyo kumtangaza John Pallagyo kupita bila kupigwa na kuteuliwa kuwa mbunge Wa jimbo la Arumeru mashariki .
Kwa upande wake mgombea wa chama cha Demokrasia Makini Simoni Paul Ngilisho amesema kuwa jambo kubwa lililosababisha chama chake kushindwa katika kuchukua nafasi ya ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki ni kwamba wananchi hawana imani nao hivyo kupelekea kukosa wadhamini 31 ili kukamishisha sheria ya NEC.
Nae Juma Mohameda mgombea wa chama cha ADATADEA amesema alitekeleza matakwa yote ya kisheria na akaridisha fomu lakini zikagundulika zinamakosa, hivyo amesema watashirikiana na mbunge mteule aliyeteuliwa wa CCM kwaajili ya shughuli za maendeleo Jimbo la Arumeru Mashariki
Nitajipanga kwa awamu ya mwisho 2020 ili kuhskikisha chama changu kinapata nafasi ya kuongoza katika jimbo hili. Alisema Mohamed
Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi Pallagyo amesemaa anawashukuru viongozi wake wa chama kumpitisha katika ngazi ya wilaya hadi Taifa.
Amesema atashirikiana na viongozi wenzake na viongozi wa jimbo kuhakikisha kuwa wanaondoa kero ambazo wananchi wamekuwa wakizipitia
Amesema jimbo hilo limekuwa nje ya mfumo kwa muda mrefu 1995 kwa muda wa miaka 5,mtu wa kusemea matatizo ya eneo husika alikuwepo kutoka NCCR lakini hakuonekana tangia alipochaguliwa, 2012 hali ikaendelea kuwa mbaya, 2015, kwa baraka hizi nitajitahidi nitamlilia mhe. Rais, hatuna barabara king'ori kwenda Leguruki,Akeri, maji-Malula, siku Rais alikuja kutuomba kura alituahidi km 5 za lami tutaanzia hapo. Alisema Pallagyo.
Post A Comment: