Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika
la Kimataifa la nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) Kanda ya Afrika Prof
Shaukat Abdulrazak Ofisini kwake Jijini Dodoma, leo tarehe 13 Machi 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Mkurugenzi
wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) Kanda ya
Afrika Prof Shaukat Abdulrazak akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) Jijini Dodoma, leo tarehe 13 Machi 2019.
Wataalamu
mbalimbali kutoka Wizara ya Kilimo sambamba na Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifatilia mazungumzo kati ya Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa
la nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) Kanda ya Afrika Prof Shaukat
Abdulrazak Ofisini kwake Jijini Dodoma, leo tarehe 13 Machi 2019.
Wataalamu
mbalimbali kutoka Wizara ya Kilimo sambamba na Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifatilia mazungumzo kati ya Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa
la nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) Kanda ya Afrika Prof Shaukat
Abdulrazak Ofisini kwake Jijini Dodoma, leo tarehe 13 Machi 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 13 Machi 2019 amekutana na
kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la nguvu za
Atomiki Duniani (IAEA) Kanda ya Afrika Prof Shaukat Abdulrazak.
Katika
Mkutano huo uliotuama kwa masaa kadhaa katika Ukumbi wa Wizara ya
Kilimo Jijini Dodoma Waziri Hasunga amemueleza Prf Shaukat kuwa serikali
ya Tanzania inaendelea na mchakato wa kubaini wafanyabiashara wanaouza
mbegu feki kwa wakulima kwani wanasababisha hasara kwa wananchi na Taifa
kwa ujumla wake.
Alisema
Tanzania ni miongoni mwa nchi Duniani ambazo wananchi wake wa wamekuwa
wakiuziwa mbegu feki jambo ambalo serikali ya awamu ya tano inayoongozwa
na Mhe Rais Dkt john Pombe Magufuli imetilia mkazo kadhia hiyo na
watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kadhalika,
Waziri Hasunga alisema kuwa pamoja na Wizara ya Kilimo kuendelea na
mchakato wa kuboresha kilimo kwa kutumia teknolojia mpya lakini bado
inakabiliwa na uuzwaji wa viuatilifu feki jambo ambalo limefifihisha
juhudi za wakulima kwa muda mrefu.
“Wananchi
wetu wanajitahidi kulima kwa kiasi kikubwa lakini kumekuwepo na
changamoto kubwa ya Viuatilifu na Mbegu feki jambo hili hatuwezi
kuliacha kamwe hivyo hivi karibuni nimetangaza kiama na wafanyabiashara
wanaosambaza tutakapowabaini tutawachukulia hatua kali sana” Alikaririwa
Mhe Hasunga
Katika
hatua nyingine alieleza kuwa wakulima wengi nchini wamekuwa wakitumia
mazao yao kama mbegu badala ya kutumia mbegu mpya jambo hili linapunguza
kwa kiasi kikubwa ufanisi katika uzalishaji wa mazao.
Akizungumza
katika mkutano huo Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la nguvu za
Atomiki Duniani (IAEA) Kanda ya Afrika Prof Shaukat Abdulrazak alisema
kuwa kukutana na waziri wa Kilimo nchini Tanzania kumeimarisha maradufu
ushirikiano ambao umeanzishwa kwa muda mrefu na shirika hilo.
Alisema
kuwa mradi wa nguvu za Atomiki Duniani katika Kanda ya Afrika
unahusisha nchi 45 ambapo unajikita katika uhusiano wa ushirikiano
katika mazao mbalimbali yanayozalishwa.
Alisema
katika Visiwa vya Zanzibar Shirika hilo limesaidia kutatua changamoto
kwa kuteketeza magonjwa yote yanayoambukizwa na Mbung’o.
MWISHO
Post A Comment: