Baada ya kusambaa kwa taarifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa afisa wa ubalozi wa Syria nchini Tanzania ameshambuliwa na kuporwa na watu wasiojulikana, hatimaye serikali imethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi kupitia ukurasa wake wa Twitter, imeeleza kuwa imepata taarifa hizo na kudai kuwa vyombo vya usalama vinafuatilia suala hilo na baadaye serikali itatoa taarifa kamili kuhusu jambo hilo.
Umma unaarifiwa kuwa vyombo vya dola vinafuatilia taarifa za Afisa Ubalozi wa Syria nchini kushambuliwa, kuporwa. Taarifa kamili itatolewa,“amesema Dkt. Abbas .
Taarifa za awali zinadai kuwa afisa huyo kwa sasa amelazwa katika hospitali ya Agha Khan akipatiwa matibabu kufuatia shambulio hilo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: