Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalim waliwasili kituo Kikuu cha polisi Dar es salaam hadi wanatoka kituoni hawajahojiwa chochote.

Wakili Alex Masaba akiongea na Waandishi wa habari mara baada ya Mwenyekiti huyo kuripoti amesema kuwa “Haiwezekani mtu anafika polisi anakaa tu kwenye makochi ya central bila kuambiwa kitu chochote.“

Viongozi hao wametakiwa kuripoti tena Alhamisi ya tarehe 22 mwezi wa 3 mwaka huu, Waliotakiwa kuripoti Polisi ni pamoja na Katibu Mkuu Chadema, Vicent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika
Share To:

msumbanews

Post A Comment: