Mbunge wa Nzega (CCM), Hussein Bashe ameshindwa kuvumilia matukio mbalimbali yanayojitokeza katika ardhi ya Tanzania na mwisho ameamua kuandika barua yenye hoja binafsi kwa Katibu wa Bunge ili kuundwe kamati ya teule ya uchunguzi.
Bashe ametoa kauli hiyo dakika chache zilizopita kupitia ukurasa wake maalum wa kijamii na kuungwa mkono na wananchi kupitia 'comment' kwa uamuzi huo aliouchukua huku baadhi ya viongozi wa upinzani wakimpinga na kumuita mnafki kwa anachotaka kukifanya.
"Leo asubuhi nimewasilisha kwa Katibu wa Bunge barua ya kusudio la kuwasilisha hoja binafsi ya kuunda Kamati teule ya Bunge kuchunguza matukio mbalimbali yanayoonesha kutishia umoja, usalama na mshikamano wa Taifa letu", amesema Bashe.
Kwa upande mwingine, Mwandishi wa habari hii alipomtafuta Mbunge huyo kupitia simu yake ya kiganjani akadai hawezi kuliweka wazi suala hilo kwa sasa kwa maana amepanga kuzungumza na vyombo vya habari siku ya Alhamisi (Machi 8, 2018) ambapo ataweka bayana kuhusiana na mambo yanayotishia usalama na mshikamano wa taifa la Tanzania
Post A Comment: