MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman
Mbowe na viongozi wenzake watano wa chama hicho wamerejeshwa tena katika
Mahakama ya Kisutu, Dar leo Machi 29, 2018 asubuhi ili kuendelea na
kesi inayowakabili.
Mbowe na wenzake wamefikishwa mahakamani hapo wakitokea mahabusu ya
Segerea ambapo wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwemo kufanya
maandamano yaliyosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha NIT, Akwilina
Akwiline, Feb 16 mwaka huu, uasi na kuhamasisha chuki.
Baada ya viongozi hao kufikishwa mahakamani hapo, Mjumbe wa Kamati
Kuu ya Chadema, Edward Lowassa na viongozi wengine wa chama hicho
walifika mahakamni hapo ili kusikiliza kesi hiyo na kufanya jitihada za
kuomba dhamana kwa watuhumiwa hao leo.
Viongozi wengine waandamizi wa chama hicho wanaoshtakiwa katika kesi
hiyo ni: Katibu Mkuu Dkt Vincent Mashinji, John Mnyika, Salum Mwalimu,
Mch. Peter Msigwa na Ester Matiko ambapo wote wamefikia kwenye chemba ya
mahakama panaposikilizwa kesi hiyo.
Post A Comment: