Mbunge wa Kigoma Mjini Mh: Zitto Zuberi Kabwe amesema amesikitishwa na Taarifa ya Mkuu wa wilaya ya Mvomero ya kuwatishia Watendaji wa kata  na Wenyeviti wa vijiji kwenye Kata alizofanya ziara mwishoni mwa wiki hii.

Zitto Ameyasema hayo leo Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha Amesema  Ameshangazwa na unyanyasaji huo wa Mkuu wa wilaya ya mvomero kuwahoji viongozi wao wananchi kuhusu ziara yake wakati ziara iyo ni ya kutimoza majukumu ya kazi ya chama

Pia amesikitishwa na hatua iliyochukuliwa na jeshi la Polisi kumwita polisi Diwani wa chama cha Act Wazalendo na kuhojiwa kuhusu ziara ya Kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe iliyofanyika hivi karibuni wilayani huko.

Zitto Kabwe amesema Mkuu wa wilaya hiyo tokea ateuliwe hajawahi fika katika kijiji hicho kusikiliza kero za wananchi hivyo kuhofia wananchi kueleza changamoto zinazowakabili.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: