Makamu wa Rais, Bi Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwa na wasanii Nandy na Aslay.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana jioni aliwakaribisha nyumbani kwake wasanii wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka ‘Dogo Aslay’ na Faustina Charles maarufu kama Nandy kwa ajili ya mazungumzo mafupi na chakula cha jioni.

Kushoto ni aMeneja Chambuso na kulia ni Meneja Saleh Gadau.
Katika mazungumzo yake na wasanii hao, Bi Samia alieleza kuvutiwa sana na marudio ya kibao cha SUBALKHERI kilichorudiwa na wakali hao wa Bongo Fleva hivi karibuni na kuwapa wosia wa kuendelea kufanya kazi nzuri zaidi na kujiepusha na makundi mabaya.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: