Msanii wa muziki Bongo, Ruby amemaliza tofauti baina yake na Clouds Media Group. 
Muimbaji huyo ametumia kipindi cha XXL kuwaomba radhi wale wote aliowakwaza katika chombo hicho cha habari.
“Yeyote, awe ni mwanakamati wa Clouds, team Clouds au awe ni shabiki wa nje I like to apologize guy to say sorry to my country, sorry to this management Clouds, I love them so much all I need is support mimi naamini kwamba ukiwa mjinga kwenye kila kitu utapata kujua vitu vingi sana,” amesema Ruby.
“Nilikaa nikamuomba Boss wangu Ruge samahani, mimi ni mdogo wewe ni mkubwa, of course kwa chochote kile mimi ndio nakosea,” amesema.
Clouds Media Group walikuwa wamesitisha kucheza nyimbo za msanii huyo kutokana na tofauti zao, hivyo sasa nyimbo zake zinachezwa na inaelezwa tangu November mwaka jana ilitolewa ruhusu kwa ngoma zake kuchezwa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: