Nabii Tito (kushoto) akizungumza na Kanumba, katikati ni mdogo wa Kanumba, seth Bosco.

KAMA ulikuwa hufahamu, basi nakujuza kuwa Onesmo Machibya anayejiita Nabii Tito aliwahi kukutana na kufanya mazungumzo na aliyekuwa nyota wa Bongo Movies, Steven Kanumba enzi za uhai wake ambapo walizungumza mambo mengi ikiwemo mikakati ya nabii huyo kufungua kanisa lake.

Tito na Kanumba wakifurahia jambo.

Tukio hili lilitokea Mei 19, mwaka 2010 jijini Dar es Salaam ambapo Kanumba alikuwa na mdogo wake, Seth Bosco, kama picha zinavyoonyesha.

“Nimekutana na nabii Tito ambaye amekuwa maarufu sana kutokana na mawaidha yake anayopita barabarani akihubiri akasema alikuwa akinitafuta sana mara baada ya kukutana na swahiba wangu Ray hivyo akasema ilikuwa bado mimi.

Kanumba akiagana na tito.

“Ameseme lengo lake kuonana na mimi lilikuwa kunieleza kwamba anatafutwa sana kuuawa na kuna watu wanamtishia maisha yake hivyo akaniambia kwa kuwa muda wowote yeye anaweza kutoweka duniani iwe kwa kuuawa au kimaajabu anaomba eti iwapo atatoweka basi mimi The Greatniendeleze mafundisho yake kwa jamii nzima kulingana na imani yake.

“Nabii Tito alinambia kuwa yuko karibu kufungua kanisa lake ambalo waumini wote lazima wawe wanakunywa pombe maana ni tiba ya magonjwa mbalimbali ukiwemo ukimwi. Anadai hata Biblia kwa mujibu wake haijakataza sema watu wanazidisha kuliko kile kiasi kilichozungumzwa …hapa alinifunulia Biblia Timotheo 5:25.
“Kushikana mkono na Nabii Tito haimaanishi kuwa nilimsapoti au kumpinga kwa mahubiri yake bali nilimsikiliza tu.


“Swali la kwanza nililomuuliza ni; 
The Great: Inasemekana wewe ni nabii wa uongo?

Nabii Tito: Ni uongo gani ninaosema wakati kila kitu kimeandikwa katika biblia takatifu? Kunywa pombe si dhambi, kwenda disco si dhambi, dhambi ya ZINAA kwa mwanaume haimuhusu ndiyo maana mwanaume hana talaka, kutumia CONDOM ni dhambi kubwa sana maana tendo la ndoa si starehe bali ni uumbaji (creation) hivyo unapotumia condom na kutupa ina maana unaua viumbe aliokupa MUNGU,” alisema Kanumba.

Kanumba aliendelea kusimulia kuwa Tito alimwambia kwamba, kuwa na wanawake wengi si dhambi Mungu anapenda na kutolea mfano wa Biblia kuwa Mfalme Suleiman aliyekuwa na wanawake wengi lakini bado alikuwa ni kipenzi cha MUNGU huku akisema yeye Nabii TITO  mwenyewe ana wake watatu ambapo wawili walikuwa DAR, na mmoja ARUSHA.
Aidha, Tito alisema ana mpango wa kuongeza wake mpaka wafike saba. Pia alikuwa na watoto saba.
Nabii Tito anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma kwa tuhuma za kudhalilisha dini na kutumia Biblia kufanya vitendo vilivyo kinyume na imani anayoitangaza ambapo jeshi hilo lilibaini ana matatizo ya akili na kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa huo, Milembe kwa ajili ya vipimo zaidi na matibabu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: