SeeBait
Leo January 16, 2018 wafanyabiashara wawili Kalrav Patel na Kamal Ashar wamehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutumikia miaka 2 jela au kulipa faini ya Sh.milioni 64,  ambapo pia wametakiwa kulipa Sh.Milioni 694 baada ya kuisababishia hasara TCRA.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambapo amesema mahakama hiyo imewatia hatiani washtakiwa hao katika makosa saba yanayowakabili.

Hakimu Mashauri amesema katika kosa la kwanza la kula njama, washtakiwa wanahukumiwa kwenda jela miezi 12 ama kulipa faini ya Sh.milioni 2 kwa kila mmoja.

Pia katika kosa la pili hadi la saba, Hakimu Mashauri amesema washtakiwa hao wamehukumiwa kwenda jela miaka 2 ama kulipa faini ya Sh.milioni 5 kwa kila mmoja.

Pia Hakimu Mashauri amesema Mahakama hiyo inawaamuru washtakiwa hao kulipa Sh.Milioni 694 ikiwa ni fedha zinazotokana na hasara waliyoisababisha kwa TCRA.

Katika mashtaka yao, wanadaiwa kuwa katika maeneo ya Dar es Salaam na Zanzibar walikula njama ya kutaka kusafirisha vifaa vya mawasiliano bila kibali.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: