Mjasiriamali na Mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo amesema hana mpango wa kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Jokate ameiambia Clouds Fm kuwa anachofanya sasa hivi ndani ya chama hicho ni kuhamasisha ili kiweze kuwasaidia wananchi wa Kitanzania kwa ueledi na kwa usahihi.

“Tunajitolea kwa ajili ya chama naamini kuwa chama ndio serikali, kwa hiyo mimi nasaidia tu, naishia hapo, ni mapenzi wangu kwa vijana,” amesema.

Kuhusu kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani CCM, alijibu, “Sijui, haipo kwenye plan, haipo kwenye ramani yangu,”.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: