Msanii wa muziki Bongo, Bushoke ametoa sababu ya Aslay muziki wake kuwa na nguvu kwa sasa
Muimbaji huyo ambaye anatamba na ngoma ‘Goma la Ukae’ ameiambia Ladha3600 ya EFM kuwa wasanii wengi wanashindwa kufanya vizuri kutokana na kukopi muziki wa wenzio kitu ambacho Aslay hana.
“Huyo mwanamuziki amekuja na hiyo style mwenyewe ana nyimbo 10 na zote zina style na wanaomuiga wapo kama 1,000 na wenyewe wanapiga style hiyo, kwa hiyo watu wanachoka masikioni,” amesema.
“Ndio maana unaweza kuona Aslay alivyokuja amefanya vizuri kwa sababu amekuja na temp tofauti, kwa hiyo ukisikiliza wimbo wake unaona huyo hakuwa miongoni mwa vijana hao,” ameongeza.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: