Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole.

Chama cha Mapinduzi(CCM) kimewarudisha waliokuwa wabunge wa upinzani kugombea majimbo ya Siha na Kinondoni baada ya wabunge hao kuijiunga na chama hicho.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole imesema kuwa baada ya tafakuri na tathimini ya kina, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM na kwa mamlaka iliyokasimiwa kwake na Kikao cha Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) imemteua Dk Godwin Mollel kusimama na kugombea Jimbo la Siha, Mkoa wa Kilimanjaro na Maulid Mtulia kusimama na kugombea Jimbo la Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam.

Imesema kuwa wagombea wa ubunge wanaelekezwa kufika katika ofisi za CCM katika mikoa husika na kupokea maelekezo yahusuyo uchaguzi kutoka kwa makatibu wa CCM wa mikoa hiyo siku ya Jumanne, Januari 9 bila kukosa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: