Mbele ya Rais wa Zanzibar, Ali Mohammed Shein aliyekuwa mgeni rasmi, Azam FC wametimiza kile walichokitaka Watanzania wengi baada ya kubeba ubingwa wa Kombe la Mapinduzi.

Kikosi cha Azam FC kimeshinda kwa mikwaju 4-3 ya penalti dhidi ya URA ya Uganda katika mechi ya fainali ya Mapinduzi iliyochezwa jana usiku katika uwanja wa Amani kisiwani huko.

URA ilikuwa kama imekuwa kiboko ya Watanzania, kwa kuwa ndiyo iliitoa Simba katika michuano ya Mapinduzi, baadaye ikafanya hivyo kwa kuing'oa Yanga pia.

Lakini, tayari ilikuwa imeishinda Azam FC katika hatua za makundi. Lakini leo mambo yalikuwa magumu baada ya dakika 90 kwisha kwa sare ya bila mabao.

Dakika za nyongeza bado mambo yalikuwa magumu baada ya sare ya 0-0.

Walipoingia katika mikwaju ya penalti, kipa wa Azam FC, Razack Abarola ndiye alikuwa shujaa kwa kupangua mikwaju miwili ya Waganda hao.

Azam iliingia fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga Singida United kwa bao 1-0, huku URA wao wakitinga fainali baada ya kuichpa Yanga kwa mikwaju ya penati 5-4. Kwa ushindi huo wa jana Azam inakuwa imetwaa taji hilo kwa mara ya pili mfululizo lakini pia wakitwaa ubingwa wao wa kwanza ndani ya msimu huu
Share To:

msumbanews

Post A Comment: