Mji huo mpya wa kibiashara utakaojulikana kwa jina la BondeniCity utajengwa eneo lenye ekari zaidi ya 1,000 lililoko Oljoro, Kusini Magharibi mwa Jiji la Arusha.
Lengo la halmashauri na wawekaji ni kutekeleza dhamira ya Serikali ya kuwapatia wananchi makazi bora yaliyopangwa kisasa na kuwa na taswira ya jiji la utalii na kidiplomasia.
Mji huo wenye uwezo wa kuchukua makazi ya watu wasiopungua 100,000 utakapokamilika, juzi ulitembelewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi na Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia alisema mji wa BondeniCity ni sehemu ya mpango kamambe wa kuboresha jiji.
Mmoja wa wakurugenzi wa BondeniCity, Omar Idd Omar alisema mpango huo na utekelezaji wake utazingatia sera, sheria na maagizo yanayohusu uendelezaji wa eneo kama upimaji, umilikishaji na usambazaji wa miundombinu.
Omar alisema kuwa mradi huo utatekelezwa kwa awamu mbili; ya kwanza ni kati ya Februari na Mei.
Post A Comment: