Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Tanzania (IGP) Simoni Sirro, amewahakikishia Watanzania wote kuwa wameimarisha ulinzi na usalama  katika kipindi hiki cha sikukuu.IGP Sirro amesema hayo  Mkoani Lindi alipokuwa katika ziara ya kikazi nakuwataka watanzania washerehekee sikuuu za Krismas na Mwaka mpya kwa uhuru, kwani wao kama jeshi la polisi wamejipanga kwa ulinzi wa raia na mali zao.
"Timu zetu mbalimbali zimejipanga tumeanza doria tayari kabisa kwa kuimarisha ulinzi na usalama kwa raia wema na pia natoa tahadhari kwa wale watu ambao wanafikiria kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani hatua kali za kisheria tutachukua dhidi yao.
IGP Sirro anasema hayo zikiwa zimebakia siku chache tu kuelekea kwenye sikukuu hizo za mwisho wa mwaka.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: