Ni miaka 37 sasa imepita tangu mara ya mwisho kwa Bristol City kukutana na Manchester United katika mashindano na hii leo kwa mara nyingine tena Bristol watawakaribisha United katika michuano ya Crabao Cup.
Katika mechi ya mwisho mwaka 1980 Manchester United waliichapa Bristol kwa mabao 4 kwa 0 huku mabao ya United kwa wakati huo yakifungwa na Joe Jordan(2),Sammy McLloy na bao la kujifunga la Geoff Mereck.
Bristol sio wa kuchukulia poa hata kidogo kwani wana timu inayoonekana kujituma sana na ndio maana katika robo fainali mbili zilizopita walizocheza walishinda zote mbili, moja na Fulham na nyingine na Bradford.
Hii ni mara ya saba kwa United kufika robo fainali ya michuano hii katika mara 10 ambazo wameshiriki, na katika robo fainali sita zilizopita Manchester United wamefudhu kwenda nusu fainali mara nne.
Haitakuwa ajabu sana kwa United kutolewa na Bristol kwani United wameshatolewa mara 3 na timu ambazo hazipo ligi kuu Crystal Palace 2011-2012, Mk Dons 2014-2015 na Middlesbrough 2015-2016.
Lakini kocha wa Manchester United Jose Mourinho ndio kocha ambaye hadi sasa anafundisha soka huku akiwa ameshinda EFL mara nyingi zaidi(4), mara 3 alishinda na Chelsea huku moja akishinda na United.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: