IKIWA ni siku moja baada ya taarifa kusambaa mitandaoni kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli ametunikiwa Tuzo ya Amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) huko nchini Afrika Kusini, huku kukikosekana taarifa rasmi kutoka kwa waandaaji wa tuzo hizo.

Leo Alhamisi, Desemba 28, 2017 kupitia kipindi cha Joto la Asubuhi cha Radio  E-FM, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Gerson Msigwa amesema kuwa hana taarifa yoyote juu ya tuzo hiyo.

“Mimi sina taarifa zozote kwa sababu mtu anapotoa tuzo sio lazima awasiliane na mtu anayempa tuzo, wao wanakuwa na vigezo vyao kadri ya watu walivyowapima viongozi.“ amesema Msigwa.

“Mimi sina information zozote kwa hiyo ni vizuri mngewatafuta hao Nelson Mandela wenyewe hicho chuo waweze kuwaeleza tuzo hizo taarifa wanakuwa nazo vyuo wenyewe,“ amesisitiza Msigwa.

Hata hivyo tayari Wakfu wa Nelson Mandela nchini Afrika Kusini umebainisha kuwa haukuandaa, kusimamia wala kutoa tuzo hizo, ambazo zimeripotiwa katika vyombo mbalimbali ya habari nchini Tanzania, Kenya na Burundi jana Desemba 27, 2017.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: