Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango leo Disemba 2017, amemkabidhi Rais John Pombe Magufuli   takwimu inayoonyesha  hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), wakati wa uwekaji wa jiwe  la msingi katika ofisi za Takwimu Mjini Dodoma.

Dkt. Mpango amesema  kuwa  takwimu za utafiti uliofanywa na Ofisi ya Takwimu ya Taifa juu ya hali ya maambukizi ya VVU,  inaonyesha kuwa Mkoa wa Njombe ndo unaoongoza kwa maambukizi  ya VVU, na utafiti huo uliwahusisha   watu wenye umri wa miaka 15-49 kwa mwaka 2016-17.
"Kiwango cha maambukizi mapya bado kiko juu kwenye mikoa ya Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania ikiongozwa na Njombe 11.6%, Iringa 11.2% na Mbeya 9.2%. Mikoa yenye maambukizi ya kiwango cha chini ni Unguja 0%, Kaskazini Pemba 0%, Lindi 0.3%, Manyara 1.8% na Arusha 1.9%.", amesema Dkt. Mpango.
Mara baada ya kukabidhiwa kwa ripoti hiyo Rais Magufuli amewataka wananchi kupuuzia watu wanaotoa takwimu za uongo, na kusema kwamba wenye mamlaka ya kutoa takwimu za taifa ni ofisi ya Taifa ya Takwimu pekee.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: