Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kampuni ya Multichoice Tanzania (DStv) kuanza ofa yake kabambe ya msimu wa sikukuu, imesema inaanza kuwatunuku wateja wake kwa kuwapa chaneli za SuperSport bure kwa siku 7 kwa wateja watakaolipia huduma za DStv kabla ya kukatika
Kwa wateja wa kifurushi cha DStv Compact na DStv Compact Plus watakaofanya malipo ya kifurushi kabla ya kukatika watapata chaneli zote za SuperSport zinazopatikana katika kifurushi cha DStv Premium kwa kipindi cha muda wa siku saba (7)  mfululizo bureeee!!!
Kwa wateja watumiaji wa  kifurushi DStv Bomba  na DStv Family  wao watapata chanel zote za
SuperSport zinazopatikana kwenye Kifurushi DStv Compact na hivyo kuweza kushuhudia mechi zote za Ligi ya Uingereza (PL) na mashindano mengine makubwa kwa siku saba (7) mfululizo bureee!!!!
Akizungumzia zawadi hii Meneja wa Wateja wa Multichoice Tanzania Hilda Nakajumo amesema hii itaendelea kwa muda na ni chombeza tuu kwani baada ya muda mfupi itaanza ofa maalum ya msimu wa sikukuu. “Mara zote sisi DStv huwa tunawatunuku wateja wetu, na sasa tumeamua kuwatuza wale wote watakaolipia akaunti zao kabla hazijakatika kwa kuwapa chaneli za michezo za vifurushi vya juu” alisema.
“Kuwathamini na kuwasikiliza wateja wetu umekuwa ni utamaduni wetu endelevu. Na tutaendelea kufanya hivyo ikiwemo kurekebisha bei zetu, kutoa tuzo na ofa mbalimbali na la msingi zaidi kuhakikisha kuwa muda wote tunawapa wateja wetu huduma bora kabisa” alisisitiza Hilda na kuwataka Watanzania wote kukaa mkao wa kula kwani kuanzia Septemba 15, DStv itazindua ofa yake maalum ya sikukuu itakayokuwa gumzo hapa nchini.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: