Ndege
mbili mpya za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Q400
zinatarajia kuanza kazi wakazi wa mikoa ya Mwanza, Arusha na Zanzibar
watakuwa wa kwanza kupata ofa.
Ofisa
Habari wa shirika hilo, Lilian Fungamtama amesema safari mpya za
ndege hizo ikiwamo ya Dar es Salaam - Mwanza, nauli iliyopangwa ni
Sh160,000.
Amesema safari za Dar es Salaam - Arusha nauli yake itakuwa Sh180,00 na Zanzibar - Dar es Salaam ni Sh85,000.
“Ofa hii imetolewa na ATCL kwa safari mpya za ndege hizo,” alisema Fungamtama.
Amesema
hakutakuwa na safari ya moja kwa moja kutoka Dar es Salaam kwenda
Zanzibar, lakini itakuwapo ya kutoka Dar es Salaam -Arusha hadi
Zanzibar.
“Ndege
ya kutoka Dar es Salaam kwenda Arusha ndiyo itakayokwenda kuchukua
abiria Zanzibar haitatokea Dar es Salaam moja kwa moja,” alisema.
Akifafanua
kuhusu nauli hizo, Fungamtama alisema nauli ya kutoka Dar kwenda
Kigoma itakuwa katika madaraja mawili ambayo ilikuwapo tangu awali.
Amesema bado ndege hizo hazijaanza safari katika mikoa yote hadi hapo watakapotangaza.
Akizungumzia
safari za nje ya nchi, alisema itakuwapo ya kutoka Dar es Salaam -
Hahaya hadi Comorro ambayo nauli yake ni Sh543,950 kwenda na Sh926,650
kwa kwenda na kurudi.
“Lengo letu ni kutoa huduma nzuri itakayomridhisha kila mteja,” alisema Fungamtama.
Post A Comment: