MANISPAA ya Songea Mkoa wa Ruvuma kuanzia sasa imepiga  marufuku vitendo vya upigaji picha wodini kwa kutumia kamera au simu za mkononi katika hospitali na vituo vyake vyote vya afya.
Manispaa ya Songea inatekeleza agizo la Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma ambalo ni agizo  la Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto ambalo linaeleza kuwa kumekuwa na tabia ya wananchi kupiga picha wodini wanapofika kuwajulia hali ndugu zao ambapo baadhi ya picha wanazopiga zimekuwa zinaoneshwa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na  ujumbe wenye kupotosha jamii.Hata hivyo wakurugenzi wanatakiwa kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kuwasilisha malalamiko yao inapotokea ukiukwaji wowote katika utoaji huduma za afya.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: