WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amefunguka tena kuhusiana na utawala wa serikali ya awamu ya tano huku akisema hakuna mtu anayemtakia mabaya Rais John Magufuli katika kutimiza majukumu yake.Aidha, Lowassa aliyechuana vikali na Rais Magufuli katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 wakati alipogombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) huku akiwakilisha pia muungano wa vyama washirika vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya NCCR-Mageuzi, NLD na Chama cha Wananchi (CUF), alisema kila mtu anamtakia mema Rais Magufuli ili atekeleze vyema haki na demokrasia nchini.

Lowassa aliyasema hayo juzi usiku wakati akihojiwa Jijini Nairobi, Kenya na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), kuhusiana na hali ya kisiasa nchini.

Kabla ya juzi, Lowassa alishazungumza mara kadhaa pia kuhusiana na mtazamo wake juu ya hatua mbalimbali za Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli 

Share To:

msumbanews

Post A Comment: