Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mapema leo amezindua Chama cha Waendesha Bodaboda na Bajaj kwa Mkoa wa Dar es Salaam. 

Uzinduzi huo Umeambatana na Mpango wa Muonekano Mpya wa Madereva kwa kuwa na Kofia Nguvu 'Helment' za kisasa na Vizibao ambapo awali wengi wao walikuwa hawanazo kutokana na kutomudu gharama za manunuzi. 

Mkuu wa Mkoa ametumia nafasi hiyo kuwaomba Madereva kuwa Mabalozi kwa wenzao wanaovunja sheria za Barabarani kwa kupakiza abiria zaidi ya mmoja 'Mshikaki'. amewaomba Bodaboda kuacha kutumia Vilevi wakati wanafanya kazi zao za Usafirishaji. "Tumeongeza vituo vya Bodaboda na Bajaj kushirikiana na SUMATRA ili kurahisisha usafiri katika Jiji la Dar es Salaam" 


 

Share To:

msumbanews

Post A Comment: