Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kuhakikisha wanajenga jengo la Mionzi katika Kituo cha Afya Ngamiani kwa kutumia mapato ya ndani.


Waziri Bashungwa ameagiza hayo wakati wa ziara yake Jijini humo na kutembelea kituo hicho cha Afya kikongwe ambacho hapo awali kilishapata shilingi milioni 400 kwa ajili ya uboreshaji.


Akiwa katika Kituo hicho Mhe. Bashungwa amesema Kituo cha Afya Ngamiani ni Kikongwe  na kinahudumia watu wengi na kinasaidia kupunguza msongamano kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa sasa kinapokua hakuna huduma ya mionzi hatuwatendei haki watu wa Tanga.


Wakati umefika sasa wananchi wanaopata huduma katika Kituo hiki wakaanza kupata huduma ya mionzi na kwa sababu Jiji hili lina mapato makubwa mnaweza kabisa kujenga Jengo hilo sasa niwaelekeze kuhakikisha Jengo la utawala linajengwa haraka na linaaamza kutoa huduma.


Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Adam Malima amesema eneo la Kituo cha Ngamiani ni dogo hivyo wataangalia namna ya kubomoa baada ya majengo ya zaman ili wapate eneo ambalo wanaweza kulitumia hata kwa kujenga kwenda juu ili kuzingatia matumizi bora ya Ardhi.


Kituo cha Afya Ngamiani kilichopo katikati ya Jiji la Tanga huhudumia wagonjwa 200 - 250 kwa siku na  idadi ya wakinamama wanaojifungua kwa mwezi ni takribani 150-200.

Share To:

Post A Comment: