Mbunge wa Jimbo la Mtama na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye ameshuhudia utiaji saini wa mkataba baina ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wa Mkoa wa Lindi na mkandarasi wa Kampuni ya Halem Construction Limited kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji safi na salama wa mradi wa Nnyangao - Mtama 


Ujenzi wa mradi huo utanufainisha na kuwawezesha wananchi zaidi ya 22,000 kupata maji safi na salama ambao utagharimu zaidi ya shilingi 4,577,244,446


Mradi huo utatekelezwa jimboni humo  kwenye kata tatu za Majengo, Mtama na Nyangao zenye jumla ya vijiji 13    vya Nyangao A,  Nyangao B, Mtakuja II, Nangaka, Masasi, Majengo A, Majengo B, Mvuleni, Mihogoni, Mbalala, Makonde, Mnamba (Chluwe) na Mkwajuni


Viongozi wengine walioambatana na Mhe. Waziri Nape  ni Mhe. Shaibu Issa Ndemanga, Mkuu wa Wilaya Lindi; Mhe. Yusuph Abdalah Tipu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mtama; Waheshimiwa madiwani wa maeneo husika, watendaji wa Ruwasa na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya wakiongozwa na Mwenyekiti  comred Athumani Seif Hongonyoko.


Share To:

Post A Comment: