Bw. Salvatory Kaiza akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi za Umma na binafsi wakati wa mafunzo ya masuala ya nidhamu mahali pa kazi yaliyofanyika tarehe 03/03/2022 katika ukumbi wa maktaba ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii, kijitonyama Dar es salaam.

Wafanyakazi wa Taasisi za umma na binafsi za Elimu ya Juu wakipata mafunzo ya masuala ya nidhamu mahali pa kazi yaliyo fanyika katika ukumbi wa maktaba ya Taasisi cha Ustawi wa Jamii.

Wafanyakazi wa Taasisi za umma na binafsi za elimu ya Juu wakipata mafunzo ya masuala ya nidhamu mahali pa kazi yaliyo fanyika katika ukumbi wa maktaba ya Taasisi cha Ustawi wa Jamii. Makamu Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa jamii taaluma prof. Sotco Claudius Komba akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi za umma na binafsi wakati wa wafunzo ya nidhamu mahali pa kazi yaliyo andaliwa na watumishi wanawake wa taasisi za Elimu ya Juu wa chama cha watumisi wa taasisi za Elimu ya Juu.

Dkt Paul Loisulie mwenyekiti wa THTU Taifa akichangia mada wakati wa mafunzo ya masuala ya nidhamu mahali pa kazi yaliyo andaliwa na watumishi wanawake wa chama cha watumishi wa Taasisi ya Elimu ya Juu. Yaliyofanyika katita ukumbi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii. Kaimu Mkuu wa Taasisi Dkt. Eventus Mugyabuso akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya juu,waliohudhuria mafunzo ya masuala ya nidhamu mahali pa kazi yaliyo andaliwa na watumishi wanawake wa chama cha watumishi wa Elimu ya Juu na kufanyika katika ukumbi wa maktaba ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii, kijitonyama Dar es salaam.

Bi. Roselyne Mathew Massaum akisoma risala iliyoandaliwa na kamati ya wanawake THTU,wakati wa mafunzo ya nidhamu mahali pa kazi yaliyo andaliwa na watumishi wanawake wa taasisi za Elimu ya Juu wa chama cha watumishi wa Taasisi za Elimu ya Juu.

Bw. Salvatory Kaiza Katibu Msaidizi Tume ya Utumishi wa Umma (kushoto), akifuatiwa na Bi Salma Fundi Mwenyekiti jumuiya ya Wanawake THTU taifa na Mwenyekiti wa THTU Taifa Dkt.Paul Loisulie.

*************************

Katibu Msaidizi kutoka Tume ya Utumishi wa Umma Ndug. Salvatory Kaiza amewaasa watumishi wanawake kutoka katika taasisi za umma na binafsi za elimu ya juu kukemea na kufichua vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa kike.

Ameyasema hayo leo tarehe 03/03/2022 katika mafunzo ya nidhamu na utaratibu wa undeshaji wa mashauri ya nidhamu sehemu za kazi yaliyoandaliwa na Chama cha wafanyakazi taasisi za elimu ya juu THTU - wanawake taifa katika ukumbi wa maktaba ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kijitonyama, Dar es salaam.

Ndg. Salvatory Kaiza amesema “nidhamu ni swala la muhimu sana kwa watumishi wa umma ili kufikia malengo ya Taasisi, ni vyema wafanyakazi kuzingatia,sheria taratibu na kanuni mahali pa kazi ili kufanikisha utendaji wa kazi katika taasisi,kulinda utumishi wetu na tumalize utumishi wetu salama pia kuwalinda watoto wetu hasa wakike walioko vyuoni” amesema Salvatory Kaiza.

Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt. Eventus Mugyabuso amepongeza mafunzo hayo kwani Mwanamke ndiye mhanga mkuu pale mtumishi wa Umma yeyote anapo adhibiwa akifanya makosa iwe yeye mwenyewe au iwe familia, hivyo ni jambo jema sana kwa mafunzo haya kuandaliwa na wanawake wa THTU Taifa ambaye Mwenyekiti wake ni mhadhiri msaidizi kutoka hapa katika Taasisi yetu ya Ustawi wa Jamii.

Kwa upande wake Prof Sotco Claudius Komba Makamu Mkuu wa Taasisi Taaluma, amewakaribisha wafanyakazi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii na watumishi wanawake wa Taasisi za elimu ya juu waliofika kushiriki katika mafunzo hayo ambayo yatasaidia katika ustawi wa nidhamu kazini na amewashukuru wote kwa kuja kupata mafunzo haya.

“Nawakaribisha sana katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii na tunashukuru kwa kuja kuendesha mafunzo haya kwenye Taasisi yetu, tunaamini mafunzo haya yatatupa mwangaza kuhusiana na nidhamu kwa wafanyakazi” amesema Prof Komba.

Kaimu mratibu Msaidizi kamati ya wanawake THTU Bi Roselyne Mathew Massam amesema mafunzo haya yameratibiwa na chama cha wanawake THTU kuelekea kwenye maazimisho ya siku ya wanawake Duniani yenye lengo la kusaidia watumishi kuelewa umuhimu wa nidhamu mahali pa kazi, kupunguza migogoro kazini na ucheleweshwaji wa rufaa kwa mfanyakazi.

Aidha Bi Roselyne Massam ameomba Tume ya Utumishi wa Umma kuongeza wafanyakazi wanaoshughulikia mashauri ya nidhamu sehemu za kazi ili kuongeza kasi ya utendaji na kupunguza ucheleweshwaji wa rufaa kwa mfanyakazi.

“Tunaomba tume iongeze watendaji ili kusaidia kuongeza kasi ya utendaji na kupunguza ucheleweshwaji wa rufaa kwa mfanyakazi,mashauri mengi yanachukua muda mrefu na inachukua muda mrefu kwa mfanyakazi kurudishwa kazini” amesema bi Roselyne.

Mafunzi hayo ni ya siku moja waliyo andaliwa na wanawake wa THTU kuelekea kilele cha siku wa Mwanamke Duniani tarehe 8 Machi 2022.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: