Ziara ya kutembelea Wananchi wa Kata na Vijiji mbalimbali ya Mbunge wa Chalinze na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete imeendelea tena leo Jumamosi Machi 05, 2022 kwa kutembelea Kata ya Kibindu.


Wakieleza masuala mbalimbali, Wananchi wa Kijiji cha Kwa-Mduma waliofika kwenye Mkutano huo wamemshukuru sana Mhe. Ridhiwani kwa namna anavyoweka nguvu kubwa kutatua migogoro na kero huku akisukuma sana maendeleo ya Kijiji chao na Jimbo kwa ujumla.


Ndugu Hussein Shafii wakati akizungumza mbele wa Mhe. Ridhiwani kwenye Mkutano huo amesema Wanamshukuru sana Mhe. Mbunge wa Naibu Waziri kwa kutatua mgogoro wa kwenye Hifadhi ya Uzigua kwenye Kijiji cha Kwa- Mduma.


Mwingine Ndugu Selemani akapongeza jitihada za Mhe. Ridhiwani kusukuma ukarabati wa barabara kila mara ikiharibika huku sasahivi ikijengwa barabara kubwa kutoka kwa Luhombe mpaka Gole ambayo Mkandarasi yuko barabarani anajenga barabara hiyo kwa kasi sana.


Wananchi wa Kata hiyo wamemshukuru sana  Rais Samia na Mhe Ridhiwani kufanikisha kujenga Kituo cha Afya Kibindu ambapo Rais Samia alileta fedha pamoja na ununuzi wa gari ya kubebea wagonjwa 'Ambulance’, na usimamizi wa Mhe. Ridhiwani uliopelekea serikali kutoa kiasi cha shilingi Bilioni 1.8 kwa ajili ya ujenzi wa  Mabwawa mawili makubwa ya Maji katika Kitongoji cha Mjema na jengine kijiji cha Kwa-Msanja ambayo yatasaidia kupeleka maji na kumaliza changamoto ya maji kwenye Vijiji vya Kata Ya Kibindu na hususan Vijiji vya Kwa- Mduma, Kibindu, na hasa kitongoji cha Kwa-Vuli na kadhalika.


Kwenye Mikutano hiyo , Wananchi pia walipata nafasi ya kueleza changamoto na kero zao ambazo papo kwa papo zilipatiwa ufumbuzi na Mhe. Ridhiwani Kikwete na Wataalamu mbalimbali wa Halmashauri ya Chalinze wakiongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri.

Share To:

Post A Comment: