Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Mej. Jenerali (Mstaafu) Hamisi Semfuko,

Jana Machi 9,2022 amekabidhi magari tisa yakiwemo Toyota Land Cruiser 'Hard Top' 5 na Suzuki Jimny, manne.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Meja Jen. Semfuko amesema gari aina ya Toyota Land Cruiser zitatumika katika shughuli za doria na utawala huku Suzuki zikitarajiwa kutumika kwenye ufuatiliaji (Monitoring) wa Wanyamapori jamii ya Faru katika Mapori ya Akiba ya Maswa na Ikorongo/Grumeti.

Meja Jen. Semfuko (mstaafu), amekabidhi magari hayo kwa Menejimenti ya TAWA iliyoongozwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Sylivester Mushi, aliyemwakilisha Kamishna wa Uhifadhi, Mabula Misungwi Nyanda.

Mwenyekiti huyo wa Bodi, akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika Ofisi za Makao Makuu, Morogoro, ameitaka Menejimenti ya TAWA kuyatunza magari hayo ili yafanye kazi kwa ufanisi iliokusudiwa.

Sambamba na kukabidhi magari hayo, Mwenyekiti wa Bodi pia amezindua ujenzi wa miundombinu ya utalii ikiwepo barabara yenye urefu wa km 42, ujenzi wa geti la kuingilia watalii na nyumba za watumishi katika Pori la Akiba Wami - Mbiki.

 

Share To:

Post A Comment: