Meneja wa Wakala huo Mkoani Tanga Mhandisi George Tarimo akizungumza jambo wakati wa mafunzo hayoi
Meneja wa Wakala huo Mkoani Tanga Mhandisi George Tarimo akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo
Meneja wa Wakala huo Mkoani Tanga Mhandisi George Tarimo akizungumza wakati wa mafunzo hayo kushoto ni Meneja wa Tarura wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene
Meneja wa Tarura wilaya ya Tanga Mhandisi Boniface Mwambene akieleza jambo wakati wa mafunzo hayo kulia ni Meneja wa Tarura Mkoa wa Tanga Mhandisi George Tarimo

 

Mchambuzi wa Mifumo Joseph Chigalula akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo
Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Sussan Uhinga akiuliza swali wakati wa mafunzo hayo
Ufafanuzi ukiendelea kutolewa

 

Mwandishi wa TBC Mkoa wa Tanga Bertha Mwambele akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Sehemu ya watumishi wa Tarura wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mafunzo hayo





A OSCAR ASSENGA, TANGA.

WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini nchini (Tarura) mkoani Tang umetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari mkoani Tanga kuhusu mfumo wa Termis wa ukusanyaji wa tozo za maesho kwa njia ya Kidigitali huku wakitakiwa kuwa mabalozi.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Meneja wa Wakala huo Mkoani Tanga Mhandisi George Tarimo alisema mfumo huo sio mpya nchini kwani umeshatekelezwa mikoa mengine huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano .

Alisema kwa maana mfumo huo sio mpya hapa nchini kwani umeshatekelezwa mikoa mbalimbali lengo kubwa la serikali ni kuhakikisha unatumika nchi nzima na wataalamu watakuwa wakitoa elimu.

Aidha alisema mfumo huo ni rafiki na rahisi ambao unawezesha mapato ya Serikali kuweza kufika sehemu husika tofauti na awali maana watakuwa hawapokei fedha mbichi kwani wenye chombo watakuwa wakilipa wenyewe kwa simu na fedha yako inafika kwenye mfuko mkuu wa serikali na baadae kurejeshwa kutengeneza barabara.

“Kwa kweli mfumo huu ni mzuri kwani ni rafiki na rahisi ambao utawezesha mapato ya Serikali kuweza kufika sehemu husika tofauti na awali na baadae kurejeshwa kutumika katika kuimarisha miundombni ya barabara”Alisema

Alisema kwenye mfumo huo mpya wa tozo za ukusanyaji wa maegesho awali Tanga walikuwa wakikusanya tozo za maegesho za magari lakini kwa sasa kutokana na mfumo na kanuni za utunzaji wa maegesho zilizotoka mwaka jana zinawataka kutoza tozo za maegesho kwenye pikipiki na vyombo vya magairi matatu bajaji na viwango vimebadilika.


Aidha alisema awaIi walikuwa wanachaji kwa siku kwenye magari kwa gari kwa sasa ambapo kuna vifurushi vya aina nne kwa saa 300 na siku nzima 1000 huku wiki ikiwa ni 5000 na magesho kwa mwezi 20000.

Hata hivyo alisema kwa upande wa pikipini kwa siku 300 na kwa wiki itakuwa 1500 wakati itakuwa ni mwezi 6000 ikiwemo kueleza kwa pikipiki zenye magurudumu matatu (Bajaji) kwa siku 500,wiki 2500 na mwezi 20000.

Hata hivyo alisema kwa mujibu wa hiyo kanuni limewataka kutekeleza zoezi la ukusanyaji kwa halmashauri za miji na wamejipanga kwenye Halmshauri za Korogwe mjini na Handeni Mjini ila huko viwango vitakuwa tofauti.

“Niwaase wananchi wa Mkoa huu na viunga vyake kutoa ushirikiano ili wasikute wanachajiwa vifurushi ambacho hukustahili kuchajiwa na zoezi hilo litafanyika kuanza saa 12 hadi saa kumi na mbili jioni kwa Jumatatu hadi Ijumaa huku Jumamosi litaanza 12.00 hadi saa saba mchana”Alisema

“Usikubali kutozwa zaidi ya saa saba siku ya Jumamosi lakini Jumapili hatufanyi kazi na siku za sikukuu”alisema

Hata hivyo aliwasihi wananchi wa mkoa wa Tanga watoe ushirikiano pale ambapo watakapopata changamoto kwa sababu ni mfumo mpya hivyo wasisite kufika kwenye ofisi zao na wale wanaotoza kwa njia ya kidigidali wamepewa mafunzo.

“Kwa kipindi chote tutakapokuwa Tanga wataalamu watakuwa katika maeneo ya Msingi kutoa taarifa na kuelekeza wananchi na wadau zoezi hilo litakuwa endelevu hadi hapo watakapokuwa na uelewa wa pamoja lengo ni wananchi waifurahi hiyo huduma “Alisema



Mwisho.



Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: