Mkurugenzi wa Chama cha Wanawake Wahasibu (TAWCO)  CPA Tumaini Lawrence akizungumza na wakati hafla ya Wiki ya Fedha Duniani iliyoratibiwa na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampas ya Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Uhasibu na Fedha (IAA) Kampas ya Dar es Salaam  CPA Faiza Msheri akizungumza kuhusiana na umhimu wa wiki ya fedha iliyofanyika katika hicho jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Wiki ya Fedha Duniani wa IAA CPA Vaileth Maira akizungumza kuhusiana na wiki hiyo na umhimu wadau kupewa elimu ya masuala ya Fedha jijini Dar es Salaam.
 


Wanafunzi pamoja na meza ya mgeni rasmi wakionesha vipeperushi vya Wiki ya Fedha Duniani katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampas ya Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi na waandaji wa Wiki ya Fedha Duniani wakiwa nyuma ya mgeni rasmi.


Vijana na Wanafunzi wa Shule za Sekondari  pamoja na Msingi  wametakiwa kujengwa katika masuala ya fedha ili kusaidia kufanya maamuzi sahihi kwa kujiletea maendeleo.

Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Chama cha Wahasibu Wanawake (TAWCO ) Tumaini Lawrence wakati wa maadhimisho ya Wiki Fedha Duniani ambayo imeratibiwa na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampas ya Dar es Salaam ,amesema kuwa suala la fedha linatakiwa kila mmoja ajue kwani asilimia 54 ya watu wanaopata msongo wa mawazo ni kutokana na fedha.

Amesema wiki  ya Fedha Duniani tangu kuanza kuadhimishwa lengo lake lilikuwa ni watu kupewa uelewa wa fedha kwani wakijengwa wanakuwa watu makini na hata wakiwa kazini hawawezi kuwa wala rushwa.

"Watu kuwa na uelewa wa fedha katika kufanya mipango tangu akiwa na umri mdogo ni vigumu katika umri mkubwa kuweza kupangilia fedha kwani ndio anakuwa amezipata kwa mara ya kwanza hivyo lazima jamii ielemishwe masuala ya fedha "amesema Tumaini

Tumaini amesema Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Tawi la Dar es Salaam wameona mbalimbali katika kushirikisha wanafunzi wa Vyuo , Shule za Sekondari,Msingi pamoja na wadau wa Kilimo na Mifugo kwa kuamini kuwa ndio watu kupata elimu hiyo katika kujijenga kifikra katika masuala ya Fedha.

Mratibu wa Wiki ya Fedha wa IAA Vaileth Maira amesema katika wiki hiyo itakuwa yenye mafakio ya kuwajenge a uwezo wadau pamoja na kuwa na mjadala wa masuala ya fedha.
Share To:

Post A Comment: