Na,Jusline Marco;Kilimanjaro


Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 37 kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha Umahiri kwa ajili ya utoaji wa mafunzo pamoja na ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme katika kampasi ya Chuo cha Ufundi Arusha Kikuletwa katika mradi wa EASTRIP.


Kituo cha kikuletwa ambapo kinakusudiwa kuwa kitivo cha ufundishaji umahiri wataalam wa masuala ya umeme kilichopo Mkoani Kilimanjaro kinatarajiwa kukamilika mwakani mwezi juni ambapo tayari mikakati ya ujenzi huo umekamilika.



Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kigaigai wakati alipotembelea eneo hilo la mradi amekitaka Chuo cha Ufundi Arusha kampasi ya Kikuletwa  kuepuka kuwa sehemu ya migogoro ya ardhi katika maeneo yao na kumeuaka uongozi wa chuo hicho kufuatilia hatimiliki itakayo wasaidia kulinda eneo hilo lisivamiwe.





Vilevile Kigaigai  ametoa muda wa miezi mitatu kwa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Hai kuhakikisha wanakamilisha mchakato wa hatimiliki ya eneo lote la mradi huo na kuagiza watu wa mazingira katika Mikoa ya Kilimanjaro,Arusha na Manyara kujitajidi kulinda mazingira ya maeneo ya mradi huo ili yasiharibike.




Mbali na kutoa maagizo hayo Kigaigai ameuhakikishia uongozi wa chuo hicho usalama katika utekekezaji wa mradi huo kwa muda wote huku akisisitiza kwamba eneo hilo la mradi kwa sasa ni eneo la kimkakati na serikali  italilinda muda wote.






Kwa upande Kaimu Mkuu wa chuo cha ufundi cha Arusha,Dkt.Musa Chacha amesema lengo kuu la kutekeleza mradi huo ni kuzalisha wataalamu ambao watakwenda kufanya kazi katika bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere.





Aidha Dkt. Chacha amesema tayari wameshaanza kutekeleza mradi huo kwa kukarabati maeneo ya zamani ndani ya kituo hicho na kuajiri watumishi mbalimbali na kusema kuwa umeme ambao utakuwa unafuliwa katika kiyuo hicho utakuwa u atumika katika ufundishaji.


 




Mwenyekiti Kamati ya utekelezaji wa mradi wa Kikuletwa Dkt. Erick Mgaya amesema mradi huo ambao umelenga ujenzi wa kituo kwa ajili ya mafunzo pamoja na ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme utagharimu jumla ya shilingi bilioni 37 ambapo tayari mradi umeanza kutekelezwa na unatarajiwa kukamilika juni 2023.





Mbali na kutoa maagizo hayo Kigaigai aliwahakikishia  usalama watekekezaji wa mradi huo kwa muda wote huku akisisitiza kwamba eneo hilo la mradi kwa sasa ni eneo la kimkakati na serikali  italilinda muda wote.



Mwenyekiti wa kamati ya utekelezaji wa mradi huo,Dkt Eric Mgaya alisema jumla ya  kiasi cha zaidi ya sh,37 bilioni zinataraji kutumika kugharamia mradi wa kufua umeme wa Kikuletwa uliopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.





Vilevile Dkt.Mgaya  amesema fedha hizo zimetolewa kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka benki ya dunia ambapo zitagharamia mradi huo ambao utaeta tija na mapinduzi katika sekta ya nishati ya umeme hapa nchini huku akisisitiza mradi huo utaenda kuzalisha wataalamu wa masuala ya umeme .

Share To:

Post A Comment: