Chuo kimeboresha miundombinu katika mabweni ya Wanafunzi, madarasa pamoja na ofisi za Wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na kuweka umeme jua kwenye mabweni na kwenye barabara, Katika Kampasi ya Kivukoni mshauri elekezi kwa ajili ya ujenzi wa maktaba kubwa yenye uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 2,500 pamoja na ukumbi wa mihadahara wenye uwezo wa watu 1000, mshauri ameshakamilisha michoro yote na mchakato wa kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi unaendelea.


Katika Kampasi ya Karume, kazi ya ujenzi wa mabweni yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 1536 unaendelea vizuri. Kwa mujibu wa mkataba ujenzi unatakiwa kukamilika tarehe 22/12/2022.


Katika kampasi ya Karume Mshauri elekezi tayari ameshakamilisha michoro kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Wafanyakazi 30. Aidha mchakato wa kumpata mkandarasi wa kujenga nyumba hizo unaendelea.


Katika tawi la Pemba, Mshauri elekezi tayari ameshakamilisha kuandaa Mpango kabambe (Master Plan) wa eneo la Chuo, Usanifu wa majengo (structural design) kwa ajili ya madarasa na mabweni, usanifu majengo (Architectural Design) kwa ajili ya madarasa, Sera ya Uthibiti Ubora imehuishwa ili kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa ni bora na yenye viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa.


Zoezi la kuandaa mitaala mipya na kuhuisha mitaala ya zamani limekamilika ili kuwa na mitaala inayozingatia mahitaji halisi ya kitafa na kimataifa.


Chuo kimetenga bajeti kwa ajili ya kuwawezesha wahadhiri kufanya tafiti mbalimbali zenye maslahi kwa Chuo na taifa kwa ujumla na kuwa tayari Wahadhiri wamejengewa uwezo wa kuandika maandiko ya utafiti na machapisho.


Chuo kimefanikiwa kutoa mafunzo ya Uongozi na Maadili kwa viongozi na watendaji kutoka Taaisisi mbalimbali pamoja na wanafunzi wa Chuo, na kufanya idadi ya waliofuzu mafunzo hayo kuwa zaidi ya 4,000.Kivukoni udahili umeogezeka kutoka wanafunzi 9,754 mwaka 2020/2021 hadi 11,184 mwaka 2021/2022. 

Aidha Katika kampasi ya Karume – Zanzibar pia udahili umeongezeka kutoka Wanafunzi 1,659 mwaka 2021/2022 hadi 2,302 mwaka 2021/2022. 


Na Tawi la Pemba kwa mwaka 2021/2022 ina wanafunzi Chuo kimefanikiwa kuongeza udahili wa Wanafunzi ambapo katika Kampasi ya 100.


 Hivyo idadi ya wanafunzi kwa ujumla kwa sasa ni 13,586 (2021/2022)Chuo pia kimeongeza idadi ya wahitimu Kampasi ya Kivukoni udahili umeogezeka kutoka wanafunzi 3154 mwaka 2019/2020 hadi 4330 mwaka 2020/2021. 


Aidha Katika kampasi ya karume – Zanzibar pia wahitimu wameongezeka kutoka Wanafunzi 751 mwaka 2019/2020 hadi 1242 mwaka 2020/2021. Hivyo idadi ya wahitimu wote kwa mwaka 2020/2021 ilikuwa ni 5670.


Chuo kimewezesha Wahadhiri 56 kwenda kwenye mafunzo kwa ngazi mbalimbali za masomo ikiwemo Shahada ya Uzamivu, Shahada ya Uzamili, Shahada ya Awali na Stashahada.


 Hivyo, idadi ya Wahadhiri wenye shahada ya uzamivu (PhD) imeongezeka hadi wahadhiri 40 waliopo Chuoni..Hadi kufikia Februari mwaka huu Chuo kimekuwa na bunifu nyingi lakini Jumla ya bunifu 22 zimeshindanishwa kwenye maonesho mbalimbali ambapo kati ya bunifu hizo bunifu Moja ya ilishika nafasi ya pili kitaifa katika mashindando ya maonesho ya Kitaifa ya Sayansi Tekinolojia na Ubunifu (MAKISATU) na Nyingine ilishika nafasi ya nne kitaifa katika Maonyesho hayo hayo kwa mwaka 2020/21.


 Aidha bunifu zilizoshinda kitaifa ni kama Bunifu mbalimbali za wanafunzi zimeonyeswa katika Jedwali na. 1.






Share To:

Post A Comment: