Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania – TANTRADE Bi. Latifa Mohamed akikabidhi vyeti kwa baadhi ya wafanyakazi ambao walifanya vizuri katika utendaji kazi wao kwa mwaka 2021. Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania – TANTRADE Bi. Latifa Mohamed akizungumza katika hafla ya kusheherekea mafanikio walioyapata mwaka 2021 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania – TANTRADE Bi. Latifa Mohamed akipata picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Mamlaka hiyo waliopewa tuzo ya utendaji kazi mzuri kwa mwaka 2021 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania – TANTRADE Bi. Latifa Mohamed akipata picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa TANTRADE katika hafla ya kusheherekea mafanikio walioyapata mwaka 2021 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania – TANTRADE Bi. Latifa Mohamed akiburudika na muziki katika kusheherekea mafanikio walioyapata mwaka 2021 Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania – TANTRADE wakiwa katika hafla ya kusherehekea mafanikio walioyapata mwaka 2021 na kuukaribisha mwaka 2022 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania – TANTRADE Bi. Latifa Mohamed akizungumza na waandishi wa habari katika kusheherekea mafanikio walioyapata mwaka 2021. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO) ************************* NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania – TANTRADE Bi. Latifa Mohamed amewataka wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kuongeza juhudi katika kazi hasa kwa kuongeza kasi ili kuhakikisha mwaka 2022 kuwa wa mafanikio kwa TanTrade. Akizungumza katika hafla fupi ya kuwapongeza Wafanyakazi wa TanTrade na kusheherekea mafanikio walioyapata mwaka 2021, Bi.Latifa amesema sherehe hiyo ni moja ya uhamasishaji kwa wafanyakazi wa TanTrade kuhakikisha wanasonga mbele kwa kufanya kazi kwa bidii na kuongeza motisha . Amesema kupitia sherehe kama hiyo kutakuwa na zawadi mbalimbali kwa wafanyakazi ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika utendaji kazi wake ili kuongeza chachu kwa wafanyakazi wengine kuongeza bidii na kuhakikisha TanTrade inasimama imara na kuweza kukua na kufika mbali. "Tumekuwa tukikutana katika Mikutano mbalimbali ya kazi lakini hatukuwahi kufanya sherehe kujumuika kwa pamoja na tukifurahi, hivyo kupitia sherehe kama hizi zitatuweka pamoja kama jamii na kuona ni sehemu gani tunakwama na kuweza kupafanyia kazi". Amesema Bi.Latifa. Kwa upande wake Afisa Utawala TanTrad Bi.Linda Mliya amewataka wafanyakazi wenzake kufanya kazi kwa utaratibu kwa kufuata sheria na kanuni zilizopo katika kazi. Nae mfanyakazi wa TanTrade Bw.Wiliam Nyabihili ameushukuru uongozi wa TanTrade kwa kuona mchango wake katika kazi mpaka akapatiwa tuzo hivyo ataendelea kuongeza jitihada katika kazi ili kuhakikisha TanTrade inasonga mbele. "Mwaka huu nimejipanga kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kuiwezesha Mamlaka kutekeleza majukumu yake vizuri na mambo yaweze kwenda vizuri". Amesema
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: