NA RAISA SAID,TANGA

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Tanga Safia Jongo amesema watoto wenye ulemavu wa ngozi, uoni hafifi ni moja kati ya makundi yanayoathirika na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo kutengwa ,kufichwa na wengine kukatwa viungo na kuwaua.

Hivyo ameitaka jamii kubadilika na kuachana na vitendo vya namna hiyo badala yake wahakikisha wanawasaidia ili kuwawezesha kufikia malengo ambayo wamejiwekea ikiwemo ya kupata elimu.

Aliyasema hayo jana wakati Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania Mkoa wa (TPFNET) wakishirikiana na Ustawi wa jamii na wadau mbalimbali wakitoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya milioni 4 .

Msaada huo umetolewa kwa shule ya Msingi ya Watoto wenye mahitaji maalumu ya Pongwe, Wafungwa katika Gezera kuu la Maweni pamoja na kituo cha watoto yatima ikiwa ni siku moja kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia inayoadimishwa Desemba 10 kila mwaka

Alisema licha ya kufichwa watoto hao wenye ulemavu wamekuwa wakifikia hata hatua ya kukatwa viungo vyao na kuwauwa na wao ni kati ya waathirika wakaona waungane nao wawaonyeshe wako nao pamoja ili waweze kuwatia mpyo

“Kwa kweli niwashukuru wadau wetu na askari wa kike kutoa elimu kupiga ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto lakini pia kutoa msaada huu niwaambie kwamba mnayonafasi ya kuwa mawaziri au rais kikubwa mliopo shuleni wekeni bidii na juhudi kuhakikisha mnasoma kwa bidii”Alisema Kamanda huyo wa Polisi.

“Niwasihi wanangu muwe na ndoto za kuwa na maisha bora ya baadae kwa kuhakikisha mnasoma kwa bidii kwa lengo la kutimiza malengo yenu juzi tulikuwa na maadhimisho ya watu wenye ulemavu tumeona wapo viongozi wenye ulemavu hivyo tumekuja kuwatia moyo nanyi ni kundi ambalo serikali inawategemea”Alisema Kamanda huyo

Kamanda huyo alitoa wito kwa jamii kuwaangalia kwa jicho la pekee watoto wenye ulemavu wa ngozi au kutokuona kabisa kwa wazazi kutokukata tamaa kuwapeleka shuleni kwani kufanya hivyo kunawanyima haki zao za Msingi na huo ni moja ya ukatili.

“Ndugu zangu kkatili wa kijisnia, saikologia unaanza na wazazi kufarakana na mwisho wa siku wanapatika vizazi ambavyo ni watoto wahalifu hivyo Jeshi la Polisi wanapinga na wanataka watanzania kuacha suala la ukati “Alisema

Awali akizungumza Mratibu wa Dawati la Jinsia kutoka Halmashauri ya Jiji la Tanga Bertha Damas alisema kwa siku 16 za kupinga ukati wa Jinsia kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wametoa elimu ya ufahama kwa makundi mbalimbali ya Jamii kwa Jiji hilo.

Alisema changamoto kubwa iliyopo kwenye Jiji la Tanga suala la ukati wa kijisnia limekuwa ni kubwa kwenye familia wazazi wameacha wajibu wa kulinda usalama wa watoto na pia kuwanyima haki ya kuwasilikiza.

Aidha alisema wanaungana na Kamanda wa Polisi Mkoa kwenye kampeni yake ya mzazi mkanye mwanao tokea aingie wameona operesheni ya watoto Ibilisi na watu wamepokea kwa mwitiko mkubwa na kupokea elimu kwa uhitaji mkubwa baada ya RPC kuamsha amsha hivyo imesambaa kila mahali na hivyo wamekuwa wakiutumia.

Alisema wakati wa kufarakana watoto wanakosa malezi hilo ni tatizo kubwa sana Tanga hivyo watu wanapoingia kwenye mahusiano wajiulize mara mbili wanawea kudumu muda gani ili waweze kuona namna ya kuondokana na hatari hiyo.

Naye kwa upande wake Mwalimu Mkuu ya Msingi Pongwe alisema shule hiyo ilianzishwa mwaka 1946 ikiwa inachukua watoto wa kawaida na ilipofika mwaka 1976 ilianza kuchukua watoto wenye ulemavu wa macho ilianza na wavulana na baade mwaka 2006 ilianza kuchukua watoto wenye ulemavu wa ngozi

Alisema shule hiyo ina wanafunzi wasiiona 88 Kati yao wenye ualibino 64 na uoni hafifu na wasioona 24 huku wakilishukuru Jeshi la Polisi kupitia umoja wao ambao mara kwa mara wamekuwa wakiwafikia kuwajali afya za watoto wao

“Kikubwa tunawashukuru sana kwa msaada huu ambao mmeutoa kwa kweli umekidhi mahitaji ya ya watoto wetu chakula,nguo na mahitaji mengine kikubwa tuwashukuru na kuwatakia kilalaheri”Alisema

Mwisho.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: