Nteghenjwa Hosseah, Mafia 


Serikali imepeleka kiasi cha shilingi Bil. 1.9 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mafia kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Afya.


Akiwa ziarani Wilayani humo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe amesema lengo la Serikali kuleta fedha zote hizo ni kutaka kuboresha utoaji wa huduma za Afya na kuwapungizia adha wananchi wa Halmashauri hii ambayo ni miongoni mwa Halmashauri zenye mazingira magumu kutokana na kuwa kisiwani.


“Fedha tulizoleta hapa ni kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Kiegeani, Ukarabati wa Hospitali ya Wilaya sambamba na ujenzi wa zahanati kwenye maeneo mbalimbali, hii ni kuhakikisha kuwa Wananchi wa Mafia wanapata huduma bora za Afya bila vikwamza vyovyote’ Prof. Shemdoe


Akikagua maendeleo ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Kiegeani Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Grace Magembe amesema  ujenzi huo utakapokamilika utasaidia sana wananchi wa Mafia kwa kuwa utakua na huduma za upasuaji wa dharura. 


“Kituo hiki sasa kitapunguza vifo vya mama na mtoto ambao hapo awali vilikua vinatokea kwa sababu ya umbali mrefu wa kufikia kituo cha Afya kinachotoa huduma za upasuaji  lakini pia upasuaji kwa magonjwa ya wanaume utakua unatolewa hivyo wananchi wote watanufaika”.


Akizungumzia kuhusu fedha hizo Mbunge wa Mafia ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu Mhe. Omari Kipanga ameishukuru Serikali kwa niaba ya wananchi kwa fedha zote za Miradi zilizoletwa kwenye Wilaya ya Mafia kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.

Share To:

Post A Comment: