Na HERI SHAABAN


MEYA wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto ameaga mwaka 2021 kwa kugawa sembe kwa wazee Wajane 500 waliopo Vingunguti Wilaya Ilala.


MEYA Kumbilamoto aligawa  misaada hiyo leo Desemba 30/2021 kwa wajane 500 sehemu ya utaratibu wake  aliojiwekea katika kusaidia makundi maalum na kukaribisha mwaka 2022.


"  Misaada hii ya chakula imetolewa na WADAU wa Maendeleo Agro Premium ya Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia jamii " alisema Kumbilamoto.


MEYA Kumbilamoto alisema kampuni hiyo ya Agro Premium pia inawalisha  Wanafunzi elfu kumi wa Wilaya Ilala


 Kumbilamoto alisema misaada hiyo  utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan, katika utatuzi wa kero.


Amewataka viongozi na Wadau mbalimbali kuunga mkono juhudi zake katika  kuwasaidia wananchi kwa kutatua kero zao


Share To:

Post A Comment: