Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele wakati wa kufunga mafunzo hayo ya jeshi la akiba.

MKUU wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele amewataka wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la akiba Wilayani humo kutoa msaada kwa jamii na kuviishi viapo vyao.

Gowele ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya mgambo, ambapo aliwasisitiza wahitimu kuonyesha nidhamu na kushirikiana na jamii kusimamia amani badala ya kuwa wa kwanza kuleta madhara kwa wananchi.

Aidha alitoa maelekezo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji pamoja na wananchi wake kutoa ushirikiano kwa Jeshi la akiba katika nyanja mbalimbali ili kuweza kunufaika na wahitimu hao kupitia mafunzo waliyopatiwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rufiji Juma Ligomba alisema wapo tayari kutoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la akiba na kwamba watahakikisha fursa za ajira
zikitokea kwa wenye sifa kipaumbele kinakuwa kwa Vijana hao.

Naye Mshauri wa Mgambo Rufiji Kapteni Linje Mtelelah alieleza kikwazo wanachokabiliana nacho kuwa ni ushirikiano hafifu kati ya jamii na jeshi la akiba.

Mtelelah alisema hali hiyo imekuwa ikisababisha uwepo wa mazingira magumu kwa Jeshi la akiba katika ufanyaji kazi pale inapobidi kwa jamii inayowazunguka.
Share To:

Post A Comment: