Wednesday, 24 November 2021

WATAALAMU UHIFADHI MISITU WA SERIKALI WATAKIWA KUCHAPA KAZI

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack akizungumza juzi na waandishi wa habari ( hawapo pichani) ambao walikuwepo mkoani humo katika ziara ya kujifunza kuhusu utekelezaji wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu ambayo iliratibiwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu (MJUMITA) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswis (SDC)
Mkutano na waandi wa habari ukiendelea,

Afisa Uhusiano wa TFCG Bettie Luwuge akizungumza kwenye mkutano huo.

Afisa Sera na Majadiliano wa TFCG Elida Fundi  akizungumza kwenye mkutano huo.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack akizungumza na maofisa wa Mashirika ya TFCG na MJUMITA baada ya mkutano na waandishi wa habari. Afisa Uhusiano wa TFCG Bettie Luwuge na Afisa Sera na Majadiliano wa TFCG Elida Fundi.

Picha ya pamoja baada ya mkutano huo.
Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.


Na Dotto Mwaibale,  Lindi.


WATAALAMU wa Uhifadhi misitu Serikalini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii badala ya kuyategemea mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambayo yanafanya kazi hizo kwa mkataba.

Hayo yamesemwa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao walikuwepo mkoani humo katika ziara ya kujifunza kuhusu utekelezaji wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu ambayo iliratibiwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu (MJUMITA) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswis (SDC)

RC Telack alifikia hatua ya kuyasema hayo baada ya maofisa wa mashirika hayo kumuambia wamebakiza mwaka mmoja wa kutoa elimu na kuhamasisha utunzaji wa misitu katika katika mkoa huo baada ya mkataba wao kukaribia kumalizika.

"Nichukue nafasi hii kuwataka wahifadhi wa misitu wa serikali kufanya kazi kwa bidii kwani serikali iliwasomesha kwa ajili ya shughuli hiyo na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kila mwaka kinatoa wahitimu wa uhifadhi wa wanyamapori na misitu hivyo katika suala hilo hakuna wasiwasi" alisema.

Alisema wahitimu hao mafunzo yao wakiwa shuleni ni mepesi na laini kwani naye amesoma katika chuo hicho na sasa kazini kwao ni mkoani Lindi hivyo licha ya mashirika hayo kumaliza muda wao wataalamu hao waliosomeshwa na serikali watafanya kazi hiyo.

Alisema kazi ya wahifadhi hao ni kuisaidia Serikali na kuwa misitu ikiachwa ipotee kilimo kinachosemwa ndio uti wa mgongo hakitakuwepo kwani misitu ni chanzo cha mvua na kuwa  mikoa yenye misitu mingi ndiyo yenye mvua za kutosha. 

Alisema kwa Mkoa wa Lindi ambao bado una misitu mimgi ya kutosha wenye wajibu wa kuhakikisha inatunzwa ni wataalamu hao na akawataka waamuke sasa na kuelekeza nguvu zao kwenye suala zima la uhifadhi wa misitu.

Aidha Telack aliyaomba mashirika hayo kwa muda huo wa mwaka mmoja uliobaki kutoa elimu hiyo ya uhifadhi wa misitu waitumie mkoani humo kwani Tanzania ni yetu wote hivyo kila mtu anajukumu la kuilinda. 

Alisema yeye kama kiongozi mkuu wa mkoa kwa kushirikiana na watendaji wake watasimamia suala zima la uhifadhi wa misitu ili kumsaidi Rais Samia Suluhu Hassan na hatakubali kuona uhalibifu wa misitu ukifanyika.

Mashirika hayo yanatekeleza mradi huo katika Wilaya za Kilosa, Mvomero, Morogoro, Liwale, Nachingwea, Kilolo na Ruangwa katika Kijiji cha Malolo.

No comments:

Post a Comment