Khadija Kalili , Kibaha
Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Injinia Mwanasha Tumbo amesema kuwa serikali inajipanga kujenga mabweni kwenye shule mbalimbali nchini Ii kuweza kuwasaidia watoto wenye changamoto waweze kubaki shuleni.
RAS Mwanasha alisema hayo leo alipokuwa mgeni rasmi katika Kongamano la watu wasioona lililofanyika Mjini Kibaha.
"Niwahakikishie kuwa serikali iko bega kwa bega na nanyi ukiwemo fursa za kupata ajira serikalini hivyo nawahimiza wazazi kuto waficha watoto wenye changamoto kwa sababu serikali yetu ya awamu ya sita chini ya Rasi Samia Suluhu Hassan inawajali' alisema RAS Mwanasha.
Aidha alitoa wito na kuwataka jamii hiyo ya watu wenye changamoto ya kuona kuendelea kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Uviko 19 na kusisi na kusisitiza kwamba ugonjwa huo upo na kuwaambia wahamasishane Ili Kila mmoja aweze kupata chanjo.
Wakati huohuo Mkurugenzi wa Kibaha Mjini Injinia Mshamu Munde amewapongeza watu wenye changamoto ya kuona kuwa wanaongoza kwa uaminifu pindi wanapokopeshwa huku akiwamasisha waendelee kuitumia fursa ya mikopo inayotolewa katika Halmashauri zote nchini kwa makundi matatu ambayo ni wanawake,vijana na walemavu.
Mkurugenzi Munde alisema kuwa Halmashauri ya Mji Kibaha wamepanga mipango jumuishi kwa kutulia maanani walemavu wa viungo na kuzingatia watu wasioona tutawawekea vipaumbele kwani tunatambua nyie msioona mna umuhimu mkubwa katika jamii na mko katika rekodi ya kundi la kurejesha mikopo kwa uaminifu mkubwa.
"Halmashauri zote zinatoa mikopo hii hivyo changamkieni hii fursa Ili muweze kukua kiuchumi"alisema Injinia Munde.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wasioona nchini Omar Sultan Mpondela alisema wako Mkoani kwenye maadhimisho ya Fimbo Nyeupe ambayo ni kifaa kisaidizi kwa watu wasioona ambapo lengo kuu ni kupaza sauti Ili jamii iweze kutambua kuwa watu wasioona ni sawa na watu wengine.
Mpondela alisema kuwa Kongamano hili limewakutanisha viongozi wa wasioona kutoka katika mikoa yote nchini pia chama hicho kilianzishwa mwaka 1964.
Post A Comment: