NA VICTOR MASANGU,KIBAHA


Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini katika kuwakomboa vijana kuondokana na kukaa vijiweni ametoa kiasi Cha shilingi laki tano kwa ajili ya kikundi Cha boda boda zawadi shop Cha mtaa wa Mwanalugali B ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Koka ametoa fedha hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuweza kusikiliza kero na changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi wa kata ya tumbi ikiwa sambamba na kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo 

Akizungumza katika mkutano na wananchi wa kata ya tumbi Koka alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuwasaidia vijana waweze kuondokana na wimbi la umasikini na kuwaletea tija katika kuleta Chachu ya kimaendeleo.

"Mm Kama Mbunge wenu lengo langu ni kuwasaidia wananchi na wakati nipo katika kampeni zangu kwa ajili ya kuomba kura niliweza kukiahidi kikundi hiki Cha boda boda Cha Mwanalugali kukipa mtaji wa fedha ambao itawasaidia katika kazi zao,"alisema Koka.

Pia Koka alisema kwamba mbali na kunisaidia kikundi hicho aliongeza kuwa atahakikisha anaweka mikakati madhubuti ya kuwasaidia wananchi katika sekta mbali mbali ikiwemo elimu pamoja na afya.

Pia Mbunge huyo katika kuchochea Kasi ya maendeleo aliweza kuchangia kiasi Cha shilingi laki  tano kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa ofisi ya serikali ya mtaa wa boko temboni.

Katika hatua nyingine aliongeza kuwa atashirikiana na mamlaka mbali mbali ili kuweza kuwasogezea huduma za maji,umeme,pamoja na suala zima la upatikanaji wa madawa na vifaa tiba katika zahanati ili kuwapunguzia adha wananchi ya kufuata huduma mbali.

Kadhalika aliwahakikishia wananchi wa mitaa mbali mbali iliyopo kata ya tumbi kuwaboreshea zaidi miundombinu ya barabara ili ziweze kupitika kwa urahisi hasa wakati wa kipindi Cha mvua.

Nao baadhi ya wananchi waliohudhulia katika mkutano huo wamemuomba Mbunge kuwasaidia kwa Hali na Mali upatikanaji wa huduma ya nishati ya umeme pamoja na ujenzi wa kituo Cha polisi.na soko.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya tumbi Raymond Chokala  alimpongeza Mbunge huyo kwa kufanya ziara ya kutembelea miradi mbali mbali pamoja na kutekeleza ilani ya Chama kwa vitendo ikiwemo kuchangia Kasi ya maendeleo.
Share To:

Post A Comment: