Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amejumuika na viongozi wa UWT Mkoa wa Mbeya katika maadhimisho ya kilele cha UWT Taifa sambamba na kumbukizi ya Bibi Titi maadhimisho yaliyofanyika Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani mgeni rasmi akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.


Maadhimisho hayo yamejumuisha Makatibu wa UWT Wilaya zote nchini sambamba na  Madiwani wa Wilaya za Chunya,Mbarali,Rungwe,Mbeya Mjini na Vijijini .


Maadhimisho hayo yamejumuisha viongozi wote wa UWT nchini kutoka Bara na Visiwani yenye lengo la kuhimiza mshikamano katika Jumuia na Chama kwa ujumla.

Share To:

Post A Comment: