Na Elizabeth Joseph,Mbeya.


WANASIASA mkoani Mbeya wametakiwa kuacha Imani za kunyang'anywa Jimbo na vijana waliofanikiwa kimaisha badala yake waheshimu na kuendeleza juhudi za vijana hao.


Kauli hiyo ilitolewa na Ndele Mwaselela ambaye Mwekezaji na  Mkurugenzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Paradise Mission iliyopo mkoani Mbeya wakati akiongea na waandishi wa habari Wanawake kutoka mikoa mbalimbali nchini.


Alisema kuwa Wanasiasa hasa mkoani Mbeya  wamekuwa wakirudisha nyuma jitihada za vijana katika maendeleo kwa kuwatengenezea makundi ya kuwachafua vijana hao hasa wanapoona wanasaidia Jamii inayowazunguka wakidhani vijana hao wana nia ya kugombea majimbo yao.


"Ukifanya jambo kwa nia nzuri kusaidia jamii wanasema unajitengeneza kisiasa na kuanza kukutengenezea makundi mitaani kuchagua jitihada zako.........


"Hii tabia ni uoga kwa maendeleo ya vijana,wanachoongea jukwaani kuhamasisha vijana kujituma ni tofauti na matendo yao wao wanachowaza ni kuporwa majimbo yao tu na si vingine"alisema Bwana Mwaselela.


Alibainisha kuwa Wanasiasa wanapaswa kuwatambua vijana wasio katika masuala ya siasa wana miradi yao inayohitaji msaada wao kimawazo na matangazo ili kuikuza miradi hiyo.


"Wanasiasa wasituchukie bali tushirikiane katika kuikuza miradi tunayoianzisha kwani hata Serikali ina nia nzuri na vijana katika kuwainua kimaendeleo"Aliongeza kusema Bw,Mwaselela.


Aidha aliwataka vijana kutorudi nyuma wanapoamua kujiinua katika maendeleo hasa katika kusaidia jamii inayowazunguka kwakuwa uwekezaji unahitaji kusimamia misimamo na nia zao katika kufikia mafaniko waliyojipangia

Share To:

Post A Comment: