Wednesday, 6 October 2021

Naibu Waziri wa Maji achangia ujenzi nyumba ya katibu

 


Na mwandishi wetu ,chunya

Maadhimisho ya Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT)kimkoa yamefanyika katika Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya ambayo pia yamehudhuriwa na Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji.
Katika hafla hiyo Mahundi amechangia roli mbili za mawe na tofali mia tano za saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu UWT Wilaya ya Chunya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mbeya Oliva Kibona amempongeza Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa namna anavyojitolea katika shughuli mbalimbali za jumuia.

No comments:

Post a Comment